DIWANI FEKI ANASWA AKITAPELI.....APEWA KIBANO NA KUTEMBEZWA TUMBO WAZI BARABARANI...!!
Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika aliyedai ni diwani wa Kata ya Kimbangolile, Mbagala jijini Dar katika utapeli kupitia mtandao wa simu.
Mwanzo wa mchezo
Awali, paparazi wetu alipigiwa simu na mtoa habari aliyejitambulisha kwa jina la Sule akidai kuwa katika sheli ya Mwanamboka, Kinondoni kuna vijana wanaotaka kumtapeli dada mmoja wakiwa na pesa feki.
“Njooni hapa Mwanamboka kuna kijana alidai ni diwani na alitaka kumpatia pesa feki dada wa mtandao mmoja wa simu ili aingiziwe kwenye akaunti yake, njooni haraka,” alisema mtoa habari huyo.
Amani latinga Eneo la tukio
Amani lilipofika eneo hilo, lilishuhudia umati wa watu huku diwani huyo ambaye baadaye ilibainika ni feki na dereva wake wakiwa chini ya ulinzi wa raia wakisubiria polisi wafike.
Akizungumza na Amani kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema:
“Hawa jamaa walifika hapa wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Sprinter lenye namba za usajili T926 BBV. Akashuka huyu kijana akiwa amevaa kiheshima na kutoa burungutu la shilingi laki 4, akaomba aingiziwe kwenye simu yake.
“Yule dada wa mtandao wa pesa alitajiwa namba ya simu na kiasi ambacho alitakiwa kuingiza kabla ya kukabidhiwa zile pesa huku akitakiwa afanye haraka kwani ‘mheshimiwa’ huyo anataka kuwahi kikao muhimu.
“Hapo ndipo yule dada aliposhtuka, alipoziangalia zile fedha akabaini ni bandia hivyo akatoka na kuanza kuwakimbiza.
“Kwa bahati, kabla matapeli hao hawajafika mbali wakagonga gari lingine na hivyo kulazimika kushuka, ndipo yule dada akawaitia wezi na raia wakawazingira.
Baada ya kukamatwa na kushushiwa kichapo huku wakizomewa, askari waliokuwa wanalinda katika kituo cha mafuta eneo hilo waliita polisi ambao walifika na kuwachukua kisha kuwatembeza mtaani huku diwani huyo akiwa tumbo wazi, pekupeku mpaka kwenye gari.
Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi lenye namba OB/RB/10460/2013 WIZI MTANDAONI.
Awali, paparazi wetu alipigiwa simu na mtoa habari aliyejitambulisha kwa jina la Sule akidai kuwa katika sheli ya Mwanamboka, Kinondoni kuna vijana wanaotaka kumtapeli dada mmoja wakiwa na pesa feki.
“Njooni hapa Mwanamboka kuna kijana alidai ni diwani na alitaka kumpatia pesa feki dada wa mtandao mmoja wa simu ili aingiziwe kwenye akaunti yake, njooni haraka,” alisema mtoa habari huyo.
Diwani akipigwa pingu. |
Amani lilipofika eneo hilo, lilishuhudia umati wa watu huku diwani huyo ambaye baadaye ilibainika ni feki na dereva wake wakiwa chini ya ulinzi wa raia wakisubiria polisi wafike.
Umati ukiwa eneo la tukio baada ya jamaa hao kunaswa. |
Mchezo ulikuwaje?
Akizungumza na Amani kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema:
“Hawa jamaa walifika hapa wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Sprinter lenye namba za usajili T926 BBV. Akashuka huyu kijana akiwa amevaa kiheshima na kutoa burungutu la shilingi laki 4, akaomba aingiziwe kwenye simu yake.
“Yule dada wa mtandao wa pesa alitajiwa namba ya simu na kiasi ambacho alitakiwa kuingiza kabla ya kukabidhiwa zile pesa huku akitakiwa afanye haraka kwani ‘mheshimiwa’ huyo anataka kuwahi kikao muhimu.
...Safari ya kuelekea kituoni |
.
“Baada ya kuingiziwa pesa kwenye simu, yule diwani feki alibwaga lile burungutu na kuondoka kwa kasi kuelekea kwenye gari kisha akamuamuru dereva aendeshe kwa kasi.“Hapo ndipo yule dada aliposhtuka, alipoziangalia zile fedha akabaini ni bandia hivyo akatoka na kuanza kuwakimbiza.
“Kwa bahati, kabla matapeli hao hawajafika mbali wakagonga gari lingine na hivyo kulazimika kushuka, ndipo yule dada akawaitia wezi na raia wakawazingira.
Diwani feki akiwa kifua wazi pamoja na mwenziye wakiongoza njia kuelekea kituoni. |
Polisi waitwa

0 comments: