Showing posts with label siasa. Show all posts

FREEMAN MBOWE ATIWA MBARONI KWA MARA NYINGINE TENA

0 comments

Mwenyekiti wa Taifa Chadema na Kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe le amekamatwa na Jeshi la polisi nchini na kuwekwa chini ya ulinzi mkali  kwa takribani masaa matatu.

Taarifa zinadai kwamba, Mbowe alitiwa nguvuni na polisi  baada ya kuwatuhumu  kuhusika na mlipuko wa bomu la arusha katika mkutano wa CHADEMA.

Kuachiwa huru kwa Mbowe kumetokana na majadiliano ya kina kati ya polisi na mawakili wake ambao wa wamekubali  kujibu kwa maandishi ni kwa nini Mbowe aliwatuhumu polisi kwa mlipuko huo.

Read More »

WALIOWAUA WANAJESHI WA TANZANIA WATAJWA.....NI KUNDI LA "JANJAWEED" LINALOUNGWA MKONO NA SERIKALI YA SUDAN

0 comments
WAKATI miili ya wanajeshi saba ikiwa imeagwa jana katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, imeelezwa kuwa kundi la Janjaweed linaloungwa mkono na serikali ya Sudan ndilo lililowavamia na kuwaua askari hao nchini humo  na kuwajeruhi wengine 17 .
Wanajeshi hao wa Tanzania ambao walikuwa ni sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), walifanyiwa unyama huo Julai 13, mwaka huu katika eneo la kusini mwa Darfur, nchini Sudan.

Kiongozi wa moja ya makundi ya wapiganaji la Sudan Liberation Movement (SLM), Minni Mannawi ameibuka na kuwatuhumu wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo na ametaka ufanyike uchunguzi wa kimataifa.
Katika mahojiano yake na Gazeti la Sudan Tribune alipokuwa anahudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu namna ya kupata amani ya kudumu nchini Sudan uliofanyika jijini Geneva Uswisi wiki iliyopita, alikanusha kuwa kundi lake linahusika na shambulio hilo.
 



“Tuna uhakika shambulio lililofanywa dhidi ya walinzi wa amani wa Unamid liliandaliwa na kutekelezwa na Janjaweed, tuko tayari kutoa ushirikiano kwa chombo maalum cha kimataifa kitakachoundwa kufanya uchunguzi kuhusu tukio hili…Nashauri serikali (ya Sudan) isishiriki katika uchunguzi kwa sababu itaficha ukweli,” alisema Mannawi.

Aliongeza kuwa wanamgambo hao waliowashambulia wanajeshi wa kulinda amani hivi sasa wanakabiliwa na ukata wa hali ya juu na kukosa vifaa kwa sababu serikali haina tena uwezo wa kuwahifadhi, hivyo wameamua kufanya matukio ya uporaji kukidhi mahitaji yao.
 
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Martin Nesirky alisema wameanza kufanya uchunguzi wao binafsi. Taarifa ya UN ilieleza juzi kuwa mashuhuda wamekuwa wakieleza mauaji hayo yamefanywa na kundi linaloungwa mkono na serikali ya Sudan.
Wakati huo huo, majeshi ya Nigeria yamejitoa kulinda amani Darfur. Hazikutolewa sababu za kufanya hivyo japokuwa UN imethibitisha.


Read More »

"WAKATI KIKWETE AKIONGOZA KUOMBA KONDOMU KWA OBAMA, MAGAZETI NAYO YALIISHIA KUANDIKA HABARI YA KUSHIKANA VIUNO".... GODBLESS LEMA

0 comments
CHAMA cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuanza kutoa mafunzo ya kujihami kwa vijana wao maarufu kama Red brigedi kuanzia Agosti mosi, mwaka huu.
Akitangaza tarehe hiyo jana wakati wa mkutano wa chama hicho uliofanyika Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini, kiongozi wa ulinzi wa chama hicho kanda ya Nyanda za juu kusini Lucas Mwampiki, alisema kuwa ameamua kuweka wazi adhima hiyo ili serikali isiendelee kusumbuka kuwa inao uwezo wa kuwazuia.
‘’Polisi msisumbuke kutafuta kuwa tutaanza lini, ni hivi, tutaanza tarehe 1, mwezi wa nane mwaka huu’’ alisema Mwampiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.
Mgeni rasmi katika mkutano huo Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na Mbunge wa Arusha mjini, alisema amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa vijana waliohitimu mafunzo ya JKT na kuachwa bila ajira ili wajiunge na mafunzo hayo.
‘’Nimekuwa nikipokea simu nyingi za vijana waliohitimu JKT na kuachwa mitaani wakiomba kujiunga na mafunzo ya Redbrigedi huku wakiuliza kiingilio’’ alisema Lema.
Alisema kuwa ijulikane kuwa mtu anapozuia demokrasia anazalisha waasi na Chadema hawapo tayari kuuawa kijinga.
Mbali na suala hilo, Lema alisema alishangazwa na uandishi wa vyombo vya habari hapa nchini katika ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama, ambapo Magazeti mengi yaliandika habari za kushikana viuno na mkewe badala ya kuandika jambo ambalo aliloijia.
‘’Waandishi wa Tanzania badala ya kuandika alichojia Obama, wao waliishia kupiga picha akiwa ameshikana na mkewe na kuweka front page huku madini yakiondoka na Rais Kikwete akiongoza kuomba Kondomu na kusaini mikataba ya kutorosha madini yetu’alisema Lema huku akishangiliwa na wananchi zaidi ya 2000 waliohudhuria mkutano huo wakiwemo viongozi wa CCM.
Aliwaambia wanachama wa Chadema kuwa waache kuwachukia wanachama wa CCM bali wawaelimishe taratibu maana hata ukitaka kupata kifaranga huwezi kununua yai dukani na kulipasua kisha ukapata kifaranga bali mpaka yai hilo liatamiwe na kuangaliwe.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi, alisema kwa sasa anakubali kuwa yeye ni ‘’Rais wa Mbeya’’ kutokana na wananchi kumkubali na kwamba CCM wasitarajie kulikomboa Jimbo la Mbeya Mjini mwaka 2015 na aliwashukuru sana Polisi wa Mbeya kwa kuacha kuisaidia CCM.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo wa kuimarisha chama katika kata ya Nsalala na Utengule Usongwe Kissman Mwangomale (KK) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mshikamano kata ya Nsalala, alisema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapaswa kujiuzulu kwasababu alitamka kuwa amechoka.

‘’Pinda anapaswa ajiuzulu maana alitamka kuwa amechoka, sisi hatujachoka tuna uwezo wa kuongoza dola aachie ngazi au afute haraka kauli yake’’ alisema Mwangomale.
Naye diwani wa kata ya Iyela ya Jijini Mbeya Charles Mkela, aliwashukuru wanachama wa CCM kumpigia kura nyingi za ndiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni na kukiwezesha Chadema kushinda.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwemo Frank Mwaisumbe ambaye ni Mratibu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini na viongozi kutoka Mbeya mjini na wilaya ya Mbozi.

Read More »

SWALA LA KODI YA LINE: HATIMAE SERIKALI YALEGEZA MSIMAMO, KUPELEKWA BUNGUNI KUJADILIWA

0 comments

Wakati Serikali imeeleza nia yake ya kuangalia upya utozaji wa kodi ya kila mwezi kwenye laini za simu za mkononi, imeeleza pia mpango wa kufunga mtambo maalumu ili kubaini malalamiko ya kampuni za simu kudaiwa kuiba fedha za watumiaji.

Katika kile kinachoonesha kusikiliza kilio cha wananchi, Serikali imesema inapitia maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau ili kuiangalia upya sheria hiyo ya kutoza kodi ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa nia ya kuwapunguzia wananchi mzigo huo.


Serikali imetoa kauli hiyo Dar es Salaam jana kupitia kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Fedha,  Dk  William Mgimwa walipozungumza na waandishi wa habari.


Dk  Mgimwa alisema hatua hiyo imekuja baada ya Serikali juzi kukutana na watoaji wa huduma za mawasiliano nchini waliofika kuwasilisha maoni yao juu ya tozo hiyo kwa nia ya kuwapunguzia wananchi wa hali ya chini ukali wake.


Hata hivyo alipoombwa na waandishi wa habari kuyaeleza mapendekezo yaliyotolewa na watoa huduma hao wa mawasiliano, Dk Mgimwa hakuwa tayari kuyataja hadharani zaidi ya kusema ni mapendekezo mazuri na rafiki kwa wananchi wa chini.



"Tulijadiliana nao mambo mengi ambayo yatatusaidia mbele ya safari namna tunavyoweza kupunguza makali hasa kwa watu wa kipato cha chini," alisisitiza Dk Mgimwa.
 

Alisema mbali ya maoni hayo ya watoa huduma za mawasiliano, pia Serikali imepokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na kuona umuhimu wa kuyapitia maoni hayo na kuyatolea majibu.
 

"Serikali imepokea maoni na mapendekezo mbalimbali na sasa tunakwenda kuyafanyia kazi na baadaye tutakuwa na taarifa ya kuwaeleza wananchi ni nini tulichokiona juu ya kodi hii.


"Tunajua wananchi wa chini wanaweza kuumia lakini si nia ya Serikali kumuumiza mtu yoyote," alisema Dk Mgimwa.

Hata hivyo kutokana na suala hilo kuwa la kisheria kutokana na kupitishwa na Bunge, Dk Mgimwa alisema Serikali itatoa majibu ya nini kimekubaliwa baada ya suala hilo kurejeshwa tena bungeni na kuamulia vinginevyo.



"Suala hili ni la kisheria, jambo lolote likipita bungeni likawa sheria hata mimi Waziri siwezi kulibadilisha lazima lifuate mkondo uleule. Vikao vya Bunge vitakaa hivi karibuni na jambo hilo litajadiliwa huko," alisisitiza Dk Mgimwa.

Makato hayo ya kodi kwa kila mtumiaji wa simu ya Sh 1,000 yalitakiwa kuanza kukatwa kuanzia Julai mosi mwaka huu, lakini Dk Mgimwa alisema kuwa kodi hiyo haijaanza kukatwa kutokana na mfumo wake kutokamilika.
 

Alisema nia ya Serikali katika kodi hiyo ni kuboresha huduma za maji, umeme na barabara hasa vijijini ili wananchi wawe na uwezo wa kufikisha mazao yao haraka sokoni na kwamba kodi hiyo si pekee kwani Serikali ilipokea mapendekezo 67 ya kodi lakini  baadhi yalionekana kutotekelezeka.

"Wazo hili lilitoka katika Kamati za Bunge kwa wabunge wenyewe na sisi hatuchuji peke yetu mawazo hayo, bali kuna Kamati ya Kodi na Kamati ya Bunge lenyewe ambazo pia zilihusika katika kutoa mapendekezo ya mwisho."

Read More »

USHUHUDA WA WANACHAMA 5 WA CUF WAKIELEZA JINSI WALIVYOTESWA NA ASKARI HUKO MTWARA

0 comments
 Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutoka (kulia) ni, Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Mtwara Mjini, Ismaili Njalu. Katibu wa Wilaya ya Mtwara mjini, Said Kulanga na Mwenyekiti wa Wilaya ya Mtwara mjini, Salum Mohamed wakiwaonesha waandishi wa habari majelaha waliyoyapata baada ya kupigwa na Wanajeshi wa Wananchi (JWTZ) katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Chama hicho Dar es Salaam.
CONTINUE READING
--------------
CHAMA cha Wananchi (CUF) kinaandaa utaratibu wa kufungua kesi mahakamani dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa watendaji wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi Mipango, Uchaguzi wa Bunge Shaweji Mketo,kwa niaba ya wanachama wenzake alisema, bado wanawasiliana na wanasheria, taasisi za haki za binadamu na mamlaka nyingine ili kupata mwongozo waweze kufungua kesi hiyo.

Mketo na wenzake watano, ni miongoni mwa watu walioonja joto ya mateso ya siku 28 kutoka kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambao wameweka kambi Mtwara kudhibiti machafuko yanayotokana na madai ya kuzuia bomba la gesi asilia lisijengwe Dar es Salaam.

Mbali na Mketo wengine ni Mwenyekiti wa Vijana Mtwara mjini Salum Mohamed, Mwenyekiti wa Mtwara mjini Salum Mohamed, Mwenyekiti wa Wilaya Mtwara vijijini Ismail Jamal,Katibu wa Wilaya Mtwara mjini Said Kulaga na dereva wa CUF makao makuu Kashinde Juma.


Naibu Mkurugenzi Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuteswa kwa wanachama watano wa chama hicho na askari wa JWTZ mkoani Mtwara. 
 -----
Akisimulia mkasa huo uliompata yeye na wenzake alisema wakiwa njiani walikutana na gari mbili za jeshi kubwa na ndogo zikiwa njia panda ya newala na mtwara mjini,na kuwasimamisha huku walitokea askari wapatao 50 vichakani na kuanza kuwapiga huku wakiwasachi mifukoni.

“Askari wa JWTZ walikuwa 50 walitusachi na kuchukua fedha zangu shilingi 85,000 na nilipoanza kuzuia fedha hizo wasizichukue ndipo walipoanza kunipiga kweli wakanivua viatu vyangu nilivyowahi kununua nje ya nchi wakavichukua na mimi kuniachia vyao vya jeshi hivi hapa ,”alieleza Mketo.

Alisema walikuwa wakipigwa na fimbo, kumwagiwa maji yaliyokuwa yamewekwa barafu na pilipili jambo ambalo liliwafanya waendelee kupata maumivu makali sana.

Mketo alisema hata hivyo kuteswa kwao ni ishara kuwa Mtwara bado inanuka damu na hakuna usalama huku wananchi wengi wakihofiwa kufariki dunia.

Hata hivyo alisema wakati wakiendelea kuwatesa alisikika mwanajeshi mmoja akisema wao wapo pale kwa ajili ya kutekeleza amri ya Waziri Mkuu aliyoitoa Bungeni kwamba wananchi watakaokaidi amri ya serikali wanatakiwa kupigwa.

Kiongozi huyo ambaye aliongea kwa masikitiko makubwa huku akiwataka wenzake kuonesha majereha kwa wanahabari alisema kuwa licha ya kuwaambia wanajeshi waliokuwa wakiwatesa kuwa amefanyiwa upasuaji mkubwa wasimpige eneo hilo hawakujali kwani waliendelea kumchapa na bakora katika eneo la mshono hadi lilipogeuka rangi na kuwa nyeusi.

Alisema kiongozi mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Mtwara mjini Salum Mohamed aliambiwa azivute ndevu zake kwa kutumia mikono na alifanya hivyo hadi haapo zilipoanza kuvuja damu ndipo wakamwambia walichokuwa wanakihitaji.

Mketo alisema vitendo hivyo ni vya kinyama na kwamba haviwezi kuvumilika hivyo serikali inatakiwa kuviangalia utendaji kazi wa vyombo vya dola kwani ni kulinda raia na si kutesa.

Hata hivyo aliilaumu serikali kwa kuvifungia vyombo vya habari mkoani humo kwa kigezo cha kwamba vinawashawishi wananchi kuandamana jambo ambalo si kweli.

Read More »

SEREKALI YAZIDIWA NGUVU KODI YA LINE ZA SIMU

0 comments
Kuna kila dalili kwamba Serikali inajipanga kufuta kodi ya Sh1,000 kila mwezi kwa wamiliki wa laini za simu baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, taasisi na baadhi ya kampuni za simu nchini.
Hiyo inatokana na kauli ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba aliyoitoa jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya Makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, CCM, kukaririwa na vyombo vya habari kikiitaka Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato badala ya tozo hiyo.
Akizungumza kwa simu jana Makamba alisema: “Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”
Alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano zinapungua... “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.
“Nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo.”
Jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema kwamba Serikali inapokea maoni ya wadau mbalimbali ili kuona namna ya kufanya marekebisho ya tozo hiyo. Hata hivyo, alisema uamuzi wa kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa Serikali bali ulipitishwa na kukubaliwa baada ya kujadiliana na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
“Hayo yalipendekezwa na Kamati ya Bunge siyo Serikali. Tena walipendekeza vyanzo 67 vya kodi likiwamo hilo la kadi za simu. Walipendekeza tukate Sh1,450 kwa mwezi, lakini sisi Serikali tukashusha hadi Sh1,000 yaani kila mwananchi akatwe Sh33.3 kwa siku na mapato yatakayopatikana yatakwenda kuboresha miradi ya maji, umeme vijijini na barabara,” alisema Dk Mgimwa.
Upinzani mkali
Wabunge wa Chadema, John Mnyika wa (Ubungo) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), wamekuwa mstari wa mbele kupinga kodi kwa kuonyesha jinsi itakavyowanyanyasa wananchi.
Mnyika amekuwa akikusanya saini za wananchi wanaopinga mpango huo wa Serikali ili awasilishe bungeni hoja ya wananchi kupinga tozo hiyo. Hadi sasa ameshakusanya saini zaidi ya 26,000.
Kwa upande wake, Zitto alisema kodi hiyo haikujadiliwa kabisa kwa kuwa iliondolewa katika mapendekezo ya mapato lakini ikarejeshwa kupitia Muswada wa Fedha ambao hutafsiri hotuba ya Bajeti kisheria.
“Kama kodi hii haikuwa kwenye hutuba, haikujadiliwa na Bunge, msingi wa Muswada wa Fedha kuwa na kodi hii haupo. Kodi hii ilirejeshwa kinyemela bungeni na kupitishwa bila mjadala.”

Read More »

CHADEMA YAJITOA KUWANIA UMEYA WA ARUSHA

0 comments

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeamua kuachana na kuwania umeya wa Jiji na badala yake kimemwomba Meya, Gaudence Lyimo (CCM), atende haki.

Katibu wa Kanda ya Kaskazini wa chama hicho, Amani  Golugwa alisema jana, kwamba Chadema haina uroho wa madaraka kama baadhi ya watu wanavyofikiri, bali inasimamia vipaumbele vya maendeleo.


Hata hivyo, kauli hiyo inapingana na nyingine ya chama hicho ya wiki hii pia, kwamba ushindi katika uchaguzi mdogo wa kata nne, ni chachu katika msimamo wa chama kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, urudiwe.

Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema, Isaya Doita, ndiye aliyenukuliwa wiki hii akisema hayo, akiamini kuwa Meya Lyimo wa CCM, alichaguliwa kimizengwe.

Baada ya Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa hivi karibuni, kimefikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha, huku CCM ikibaki na viti 12 na TLP sita.
 

Pia Chadema ina nafasi ya kuongeza kiti, kwani ina nafasi moja ya viti maalumu iliyokuwa inakaliwa na Rehema Mohamed, aliyetimuliwa mwaka 2011.

Hata hivyo, pamoja na Chadema kuongoza kwa kuwa na viti vingi vya udiwani jijini hapa, haina uwezo wa kuweka Meya, bila kushirikiana na CCM au TLP.

Chadema ikikosa ushirikiano huo, ushirikiano wa CCM na TLP, utabaki kuwa na nguvu ya kuweka Meya na naibu wake madarakani, huku Chadema ikibaki kuwa kambi ya upinzani yenye nguvu katika Baraza la Madiwani.

Golugwa alisema Chadema haina uroho wa madaraka, bali inataka uchaguzi wa Meya wa Jiji urudiwe ingawa haitaki nafasi hiyo kwa kuwa si kipaumbele chake.
 

"Tunaangalia wananchi wanafikiwaje na maendeleo tuna imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata Meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria," alisema Golugwa.  
 

"Hatuna shida na Meya wala hatuna uroho wa madaraka tunachopinga ni upatikanaji wa Meya huyo na tunamtaka afanye kazi zake kwa kusimamia misingi ya sheria na si upendeleo, tunahitaji kuona kila mwananchi ananufaika na maendeleo hadi mitaani," aliongeza.

Pia alikaririwa wakati mmoja akisema ushindi huo unaihakikishia Chadema wingi wa wajumbe katika Baraza  la Madiwani, hivyo kuwa na fursa ya kumwondoa Lyimo madarakani.

Read More »

HATIMAYE LUDOVICK JOSEPH NAYE AACHIWA KWA DHAMANA

0 comments

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Ludovick Joseph anayeshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miezi minne.

Ludovick aliachiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa Juni 10 mwaka huu.

Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 18 mwaka huu, wanakabiliwa na shitaka la kutaka kumdhuru Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky kwa kutumia sumu.

Read More »

Kwa hili la Red Brigade, CHAMA CHA CHADEMA KITAFUNGWA RASMI...!!

0 comments
Hatimaye msajili wa vyama vya siasa Nchini John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume na sheria,katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.

Msajili huyo ambaye inadaiwa ni mwanachama mwaminifu wa CCM amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.

Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.

Tangu Kamati Kuu CHADEMA itoe tamko la kufundisha vijana wake ukakamavu kukabiliana na ukatili na uharamia unaofanywa na kikundi cha Green Guard ni kama Taifa limesimama na hiyo imekuwa ni habari kuu kila mahali.Dhihirisho linaloonyesha kwamba CHADEMA ndicho chama kinachofuatiliwa habari zake zaidi hapa nchini na pia kuwa na idadi kubwa zaidi ya watanzania wanaokiunga mkono.

Viongozi ambao wameshazungumzia Tamko hilo la CHADEMA ni Rais Jakaya Kikwete,Jeshi la Polisi nchini,Viongozi wakuu wa CCM,Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia na sasa Msajili wa vyama John Tendwa.

Read More »

WEMA SEPETU: SIACHI MKOROGO HADI MADUKA YAFUNGWE

0 comments
THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.
 
Wema katika pozi linaloonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika.
Baada ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu’ kuulizwa na kujibu hivyo wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa BBM zikimuonesha akiwa nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi kwenye mwili wake.
..Mapaja ya mrembo huyo.
Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.

Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.
Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.


Read More »

BREAKING NEWZZ...CHADEMA WASHINDA KATA ZOTE NNE ZA UCHAGUZI WA MADIWANI JIJINI ARUSHA

0 comments

CHAMA CHA CHADEMA KIMESHINDA KATA ZOTE  NNE ZA UCHAGUZI JIJINI ARUSHA,UCHAGUZI  HUU AWALI ULIAHIRISHWA KUTOKANA NA SHAMBULIO LA BOMU LILILO  TOKEA KATIKA VIWANJA VYA SOWETO SIKU MOJA TU KABLA YA UCHAGUZI KUFANYIKA HAPO AWALI.TAKWIMU ZA IDADI TUTAWAWEKEA HIVI PUNDE

Read More »

MBOWE AVAMIWA USIKU WA MANANE NA POLISI NA MIKAKATI MIZITO YA KUMKATA YAFANYIKA...!

1 comments

KUNDI la polisi wenye silaha za moto juzi usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata.

Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.

Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.

Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.

Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.

RCO amsukumia RPC, akana
Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.

“Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo,” alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.

“Kwa kweli ndiyo napata taarifa hizo kutoka kwako, kuwa kiongozi huyo alifuatwa na polisi, maana silijui suala hilo hata kidogo,” alisema Wambura, naye kama alivyofanya Kimola akakata simu.

Kauli ya CHADEMA

Lakini wakati Kimola akikataa kusema chochote, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Kimola kuhusiana na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo wa juu wa kisiasa, na kudai kupewa majibu ya kushangaza.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Wilaya ya Kinondoni, Dk. Slaa alisema Kimola alijitetea akidai kwanza kukana kufika nyumbani kwa Mbowe usiku wa manane. Pili, alisema kuwa hawakwenda kumkamata Mbowe, isipokuwa kufanya naye mazungumzo na kisha wangemwacha.

Slaa alisema kitendo hicho kimewashitua na ni cha kinyama na kilichokiuka sheria za nchi na haki za binadamu. Aliongeza kwamba, daima wamekuwa wakilishutumu Jeshi la Polisi kwa kutumika vibaya kukandamiza wapinzani, lakini mara zote CHADEMA kimepuuzwa na sasa jeshi hilo limeamua kuvamia makazi ya viongozi wa kisiasa kwa madhumuni yasiyoeleweka.

Alisema haijulikani nini kingetokea ikiwa Mbowe angekuwa ndani, ikiwa walinzi wangeamua kugoma kumwachia kiongozi wao. “Tuna hofu kubwa na usalama wetu, maana pale wangeweza kufanya lolote, hata kumuua na kisha kutoa matamshi kuwa walikuwa wanajibishana kwa risasi, kama ambavyo imekuwa jadi ya askari polisi kutoa taarifa za uongo na upotoshaji wanapoua watu,” alisema Slaa.

Alisema ikiwa polisi walikuwa na shida ya kweli, wangemwita kwa njia sahihi na si kumvamia na kuingilia uhuru wake na wa familia yake kama wanakamata gaidi ama jambazi hatari.
Dk. Slaa alisema Mbowe anayo ofisi inayojulikana, na kama kweli hakukuwa na jambo baya lililopangwa na polisi hao wasingeweza kufanya uhuni kama walioufanya.

“Kama wanaweza kuvamia nyumbani kwa kiongozi mkubwa kama Mbowe wakiwa na silaha nzito, itakuwaje kwa viongozi wa kawaida na raia?” alihoji Slaa.

Kutokana na tukio hilo la kuogofya, CHADEMA imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania maana ya matukio haya ambayo yamedhamiria kuleta vurugu kubwa nchini. Kadhalika, wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuueleza umma kile kilichokusudiwa na askari wake kuvamia nyumbani kwa Mbowe mithiri ya jambazi.

Itakumbukwa pia kuwa hivi karibuni askari polisi wa Mkoa wa Arusha walivamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakiwa na silaha nzito na mbwa, na kumkamata, kisha kumtupa rumande kwa siku nzima.

Source: Tanzania Daima

Read More »

"HATUTAACHA KUWAPA MAFUNZO YA ULINZI VIJANA WETU WA 'RED BRIGADE' , TUNAJUA HIZO HI HILA ZA CCM TU "...CHADEMA

0 comments
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitarudi nyuma katika mpango wa kutoa mafunzo ya ukakamavu kupitia kikundi chake cha red brigade.

Chama hicho kimesema, tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), vyote vikiwa miongoni mwa `vyama vikubwa nchini’, vina vikundi vya aina hiyo.
 Mkurugenzi wa Oganizasheni na Mafunzo Chadema, Singo Benson, ametoa msimamo huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Tamko la Chadema kuanzisha mafunzo hayo, limeibua taharuki na kusababisha watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutaka mpango huo usitishwe.

LENGO LA MAFUNZO

Benson alisema lengo la kuimarisha kikundi hicho, ni kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwa viongozi, wanachama na wafuasi wake, ambapo CCM ikitajwa kuwa nyuma ya mashambulizi hayo.

Alisema Chadema, imekamilisha maandalizi ya mafunzo yatakayowajumuisha zaidi vijana, ili wapate mbinu za kujikinga na kuwalinda viongozi wao ikiwa ni pamoja na katika mikutano ya hadhara.

Hata hivyo, alisema mpango huo hauhusishi mafunzo ya kijeshi, akidai kwamba mafunzo kama hayo yanatolewa kwa vijana kupitia kambi maalum zinazoratibiwa na CCM.

MAKAMBI YA CCM

Benson alidai kuwa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Igunga mkoani Tabora mwishoni mwa 2011, CCM iliandaa makambi mbalimbali ya kufundisha vijana mbinu za kijeshi.

Iweje Chadema tuambiwe kuwa ni haramu kwa mwaka huu, wakati mwaka jana vijana wa CCM walifanya mafunzo na paredi ya jeshi ambayo ni hatari kwa nchi,” alihoji.

Alidai kuwa moja ya matokeo ya kambi za vijana wa CCM kule Igunga, ni kupigwa hadi kuuawa kwa Mbwana Masoud na Msafiri Mbwambo waliotokea Arumeru Mashariki.

Alidai kuwa matukio hayo yanajulikana hadi kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

AMGEUKIA MWIGULU

Benson alisema IGP Mwema anatakiwa kuanza kuwashughulikia Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba, kwa madai ya kuwa mmoja wa waasisi wa kuwabebesha vijana silaha za kwenda kushambulia raia wasiokuwa na hatia.

Hata hivyo IGP Mwema aliliambia gazeti hili jana kwamba atatoa tamko kuhusiana na sakata hilo Jumatatu ijayo.

“Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) awaeleze hao vijana wa CCM wanafanyaje hayo mafunzo yao, na wamekuwa wakitumika kuwapiga viongozi wa Chadema mbele ya polisi na hakuna hatua zinazochukuliwa,”
alisema.

Benson alisema kabla ya polisi kuanza kuwashughulikia Chadema, wanapaswa kuanzia CCM.

“Sasa Rais Kikwete aseme hao ni wajasiriamali ama wanajeshi, na kama ni wajasiriamali bunduki walizo nazo ni za nini,” alihoji Benson.

Hata hivyo, alisema kikundi chao walichokianzisha kipo kwa mujibu wa kikatiba na kwamba watafundishwa kulinda haki za Watanzania, kuwalinda viongozi na mikutano ya Chadema.

Alisema mafunzo ya kuimarisha kikundi cha ulinzi cha Chadema yatanza wiki ijayo katika mikoa mbalimbali.

Pia, Benson alisema leo, Chadema wanatarajia kuzindua msimamo wa chama kuhusu rasimu ya Katiba Mpya katika Shule ya Msingi ya Ukombozi iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.

UVCCM NAO WAIBUKA

Kwa upande wake, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), imeshutumu hatua ya Chadema kuanzisha mafunzo kwa kikundi hicho cha ‘Red brigade’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela, alisema kuwa wana wasiwasi na mafunzo yatakayotolewa na Chadema, yatakuwa na ‘sura ya kigaidi’ kwa vile yatafanyika kwa siri.
 “Tunalaani  vikali mafunzo hayo, hayana tija yoyote kwa jamii yeyote,” alisema Shigela.

Kwa mujibu wa Shigela, UVCCM haifanyi kazi za ulinzi kama `red brigade’ badala yake wanaangalia ni jinsi gani vijana wanaboreshewa huduma mbalimbali za kijamii kupitia siasa.

WAISEMEA KATIBA MPYA

Shigela aliipongeza rasimu ya Katiba Mpya kupitia Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba, kwa kuwaandaa wabunge wenye umri mdogo, tofauti na ilivyokuwa awali.

Rasimu ya Katiba Mpya inaainisha kwamba wagombea nafasi za ubunge wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 21 hadi 25,ila awe anakidhi kiwango na sifa za ubunge, hili ni jambo jema”, alisema.

Read More »

"WAPINZANI BADO NI WACHANGA SANA KUWARUHUSU WAINGIE IKULU"... MKAPA

0 comments

RAIS mstaafu, Benjamin William Mkapa, ameonyesha wazi kutoridhishwa na mwenendo wa matukio ya uvunjifu wa amani hivi sasa. 


Mkapa, mmoja wa viongozi ambao wanajiamini katika kauli zao, amewataka Watanzania kutochoka kusali na kuiombea nchi ili amani iendelee kutawala. Alisema jukumu hilo linawahusisha watu, wakiwamo viongozi wa dini ambao wana dhamana kubwa kwa waumini wao.

Mkapa alitoa kuali hiyo jana mjini Mwanza, muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi, katika jengo la ghorofa nne la Chuo Kikuu cha Sayansi, Tiba na Afya, kinachomilikiwa na Hospitali ya Bugando. “Watanzania tukitaka uchumi wetu ukue, lazima nchi iwe na amani, bila hali hiyo hakuna chochote kitakachofanyika.
 

"Ndugu zangu, nawaomba Watanzania wote kwa itikadi zao, tuwaombee viongozi wetu wa dini ili wawe na ushirikiano mzuri...na wao waliombee taifa hili, hii ni tunu tuliyopewa,” alisema Mkapa.

Pamoja na Mkapa kuzungumza kwa kifupi, alifichua siri nzito ambayo hajawahi kuitoa hadharani.

Siri hiyo, ni ile ambayo alidai wakati akiwa mdogo, wazazi walitaka asomee masomo ya upadri, lakini hakufanikiwa kufikia lengo hilo.

“Wazazi wangu walikuwa walitaka niwe padri, kwa bahati mbaya ndoto ya wazee wangu haikutimia,” alisema Mkapa.

Alisema yeye anatambua Mungu alimpangia kuongoza Watanzania, jambo ambalo lilitimia kwa kipindi cha miaka 10 ya kuliongoza taifa.

Habari zaidi zinasema, jana jioni alitarajiwa kuongoza harambee ya kukusanya Sh milioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la Chuo Kikuu cha Sayansi, Tiba na Afya, ambayo itahudhuriwa na watu mbalimbali.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bugando, Profesa Jacob Mutabaji, alisema fedha zitakazopatikana zitasaidia kazi ya ujenzi wa majengo ambayo yamegharimu Sh milioni 400.

Alisema kama jengo hilo likikamilika, litapewa jina la Mwalimu Nyerere na litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,400.

Juzi, Rais Jakaya Kikwete wakati akifunga kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), alikiri kuwapo na viashiria vya uvunjifu wa amani nchini.

Alisema katika siku za karibuni, kumeibuka viashiria vingi, vikiwamo vya watu kutangaza kuanzisha vikundi vya mgambo kwa ajili ya kujilinda.


CCM
Katika hatua nyingine, Mkapa vijana kudumisha amani na mshikamano uliopo

Akizungumza na viongozi na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, alipofika kusaini kitabu cha wageni, alisema amani ndiyo tunu ya taifa.

Mkapa alipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga ambaye aliwatambulisha watendaji na watumishi na kutoa maelezo ya hali ya kisiasa ilivyo mkoani humo.

Aliwapongeza na kuwataka kuendeleza mshikamano na umoja ndani ya chama ili vijana wasipotoshwe na wasiasa wanaotaka madaraka kwa hila na kuleta machafuko nchini kwa lengo la wao kukimbilia Ikulu kushika madaraka makubwa ya nchi, wakati bado wachanga.

Mkapa alimwagia Mbunge wa Bariadi Magharibi,John Cheyo (UDP) kutokana na kauli aliyoitoa kwenye semina ya kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), aliposema kikosi kipya kinachotaka uongozi wa Taifa hili kina wajibu wa kujifunza.

Mkapa akinukuu maneno ya Cheyo, alisema “kikosi kipya kinachotaka madaraka hakielewi na hakitaki kukili kwamba taifa hili na nchi hii inahistoria, mira na tunu zake za kutawala .

“Kwa kweli tusiombee wapinzani hawa washike nchi hawafai na haifanani kabisa na kauli, lugha na matendo yao,wanadhani wakishika madaraka makubwa ya nchi hii itasitawi zaidi kuliko ilivyo kwa CCM? Si kweli hata kijiji hawajaweza kutawala na hata hivyo wanavyotawala na majimbo hali yake ni ya hovyo”alisema

“Kizazi kipya hakitaki kukiri na kutambua kama nchi hii ina historia, mira, desturi zake na hata tunu za kutawala, ni vyema wakalitambua na kujifunza badala ya kuanza kuivuruga amani, umoja na utulivu kwa lengo la kukimbilia kushika madaraka makubwa. 


Mtanzania

Read More »

BAADA YA KUAMBIWA AMSHAURI MUME WAKE AACHANE NA SIASA.., HII NDYO KAULI ALIYOTOA JOICE KIRIA

0 comments


 
My Hubby Henry Kilewo.
 Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote.
 
My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.
 
Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa (nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).
 
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"

Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.

 
Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.
Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????

My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.

Fans Wangu wote naamini mtakuwa mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu, Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE.

Read More »

BAADA YA SERIKALI KUPITISHA SHERIA YA KILA LAINI YA SIMU KULIPIWA SHILINGI 1,000 KWA MWEZI., MH. ZITTO KABWE AFUNGUKA...!!

0 comments

 Zitto FB

Maneno haya yameandikwa na Mh. Zitto Kabwe, jana tarehe 4 Julai kupitia akaunti yake ya Facebook:
“Kodi ya Tshs 1,000 kwa mwezi Kwa kila kadi ya simu uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii. Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na Wewe mwenye simu. Kampuni ya simu inakusanya Kwa niaba ya serikali. Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili. Ni aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani kupitia muswada wa fedha, finance bill, Haieleweki. Ni skandali. Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili.”


Read More »

UPDATE: DIWANI WA CCM ALIYEMTISHIA MAISHA MH. MSIGWA AFARIKI DUNIA GHAFLA...!!

0 comments


Diwani wa kata ya nduli,aliyejimilikisha kata yote ya nduli na wananchi wote na kuwa na hati miliki ya eneo hilo,na hata kuwatuma watoto wake wa kuzaa mwenyewe wavamie mkutano wa chadema na kuwakatakata mapanga makamanda wetu wa iringa na kumuachia kilema kamanda wetu oscar mwanachuo wa ruco(kahitimu mwaka jana) kwa vile tu tulikwenda kutoa elimu ya ukombozi ktk kata yake.

 Na hatimaye sheria ikachukua mkondo wake na kushtakiwa yeye pamoja na watoto wake waliotuvamia,na aliyekuwa akitinga mahakamani na uongozi wote wa ccm wilaya-iringa na misare yao ya kijani huku akionyesha mihirizi hadharani pale mahakamani,na ambaye kesi yake inatakiwa kusikilizwa tena kesho mahakama ya mkoa-iringa,leo mchana amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla na kupelekwa hospitali ya mkoa yalikomkuta mauti,hivyo kuwaachia watoto wake kesi ya kushambulia na kujeruhi wanachama wa chadema. 

SOURCE: JAMI FORUM

Read More »

UDATE: JAJI MKUU NCHINI MISRI AAPISHWA KAMA RAIS WA MUDA NCHINI HUMO BAADA YA RAIS MORSI KUPINDULIWA..!!

0 comments

 http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/07/04/130704060338_egypt_morsi_celebration_304x171_reuters_nocredit.jpg



Jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng'oa mamlakani rais aliyechaguliwa na raia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa wingi wa kura, Mohammed Morsi. Vingozi wa kimataifa wameelezea wasiwasi kuhusu kuhusu hatua ya kumpindua mamlakani rais huyo.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.

Read More »

JESHI LA MISRI LAMUONDOA MADARAKANI RAISI MOHAMMED MORSI

0 comments
 jeshi nchini Misri limemuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali.

Akihutubia kwa njia ya televisheni jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo. 


Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.

Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi ni “mapinduzi kamili”. Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani.

Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi.

Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa.

Pia aliwasihi watu wa Misri kuepukana na ghasia. Jeshi lilimpa Bwana Morsi saa 48 kutatua matatizo ya kisiasa au kuwepo hatari ya jeshi kuingilia kati. 


Viongozi wa jeshi walisema wataweka “mwongozo” kama tofauti kati ya serikali ya ki-islam na wapinzani wake hawatamaliza matatizo yao ifikapo jumatano mchana ya tarehe tatu mwezi wa saba mwaka 2013. Tarehe hiyo ya mwisho ilipita muda wake bila ya hatua zozote kuonekana.

Bwana Morsi hakika alikataa wito wa kujiuzulu na aliapa kuendelea kubaki madarakani hata kama itamsababishia kifo chake. Pia alilalamika jeshi kutoa kitisho chake cha kuingilia kati katika matatizo ya kisiasa.

Baruti zilipaa angani kwenye umati wa watu wanaocheza na kupeperusha bendera katika uwanja wa tahriri Square mjini cairo, kiini cha ghasia za mwaka 2011 ambazo zilimuondoa Rais wa muda mrefu nchini Misri, Hosni Mubarak.

Katika wiki ilizopita maandamano yenye ghasia kati ya wafuasi na wapinzani wa bwana Morsi yameuwa takribani watu 40. 


Jeshi la Misri limetangaza kuchukua madaraka ya nchi hiyo huku likitangaza kuwa si mapinduzi lakini Mohamed Morsi si rais tena wa Misri. Tayari Saudia Arabia imetuma salamu za pongezi kwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo kwa kuchukua madaraka.

Hali ya rais Morsi ilikuwa ngumu pale wananchi wake walipoamua kuingia mitaani kumpinga siku chche zilizopita kwa maandamano baada ya kujitwalia madaraka mengi kiutawala kama mtangulizi wake.

Chanzo : sundayshomary

Read More »

MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA: CHAMA CHA CHADEMA KUFUTWA KATIKA RAMANI YA SIASA.....!!

0 comments
JOHN TENDWA




Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Mh. 'John Tendwa' ametaja kukifuta chama cha siasa cha CHADEMA endapo kitabainika kuwa ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 huko jijini Arusha na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa. Tendwa  ameyasema   hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha EATV akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp  kuhusu  hatua  zitakazochukuliwa baada ya kutokea kwa tukio hilo jijini humo.





Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu. Baada ya kauli hii ya Mh. 'Tendwa' mijadala kadhaa iliibuka kwenye mitandao hususani kwenye mtandao wa jamiiforum wakikosoa kauli hiyo.

Read More »