SIMULIZI YA KUSISIMUA: KIVULI CHEUSI, SEHEMU YA KWANZA
RIWAYA: KIVULI CHEUSI
MTUNZI: Stallone Joyfull
SEHEMU YA KWANZA
Panga boi lilikuwa linazunguka taratibu, bila kuleta dalili yoyote ya ubaridi. Sifahamu kama ilikuwa ni udogo wa chumba, ama ni hali ya hewa ya jiji la Dar es salaam? Lakini hiyo haikumsumbua mlalaji huyu mgeni, katika kitongoji duni cha keko magurumbasi.
Kitongoji kilichobeba vibaka wa simu, makahaba na zile biashara haramu; kama uuzwaji wa bangi na pombe aina ya gongo, zilipatikana kwa wingi. Karani wa nyumba ya kulala wageni, yeye alipokea bakshishi ndogo kutoka kwake. Jumamosi yake ikaelekea kuisha vizuri jioni ile ya saa kumi na mbili. Mgeni huyo aliyehifadhiwa ndani ya kofia kuukuu, alitoa masharti ya kutomuelekeza mgeni yeyote chumbani kwake. Alidai kuwa, hakuna anayemfahamu; hivyo hakuna atakayekuja kumtafuta. Hiyo haikuwa tatizo, kuitikia kwa kichwa; haraka haraka tabasamu jepesi la kiushawishi likipita juu ya papi zake. Elfu arobaini alizisunda kibindoni. Nyongeza mara nane ya bei ya kawaida. Binafsi aliiona bahati ya ngekewa, iliyomdondokea zaidi ya nyota ya jaa. Akampatia ufunguo mgeni huyo asiyeeleweka. Macho yaliyo nyuma ya miwani mikubwa meusi na mwendo wake kama anayechechemea. Yeye aliuchukua ufunguo aliopewa na kuondoka.
Ufunguo wenyewe, ulining’inizwa kwenye kibao kilichoandikwa namba ya chumba na kulifuata korido lililopanga vyumba kwa nambari zilizofuatana kimpangilio. Baada ya kuhesabu vyumba vyote, alisimama mbele ya chumba ambacho ufunguo wake alikuwa nao yeye. Aliufungua mlango na kujitoma ndani. Hakutaka kuwasha taa, kwa sababu mwanga hafifu wa jua lililoashiria kudondokea magharibi, ulimtosha kukiona kitanda. Alilala vile vile kama alivyoingia. Kitanda kikamlaki kama kilivyowalaki wengine. Kunguni waliifurahia damu yake, viroboto nao wakamchoma choma. Hakujisumbua kukishusha Chandarua, hivyo mbu walicheza gombania goli katika sikio lake.
Mara akaamka ghafla. Hakuamka kwa sababu ya usumbufu wa chumba hicho duni. Ni mlio wa simu ulioita ghafla, saa tano ya usiku. Muda ulikuwa umeenda kasi sana. Ilikuwa ni namba ya Bertha, mpenzi wake. Alijiuliza ni nani atakuwa anaitumia namba hiyo. Baada ya kuipokea, aliifahamu sauti iliyoongea kwa sauti ya hamaniko. Aliongea kiutulivu na kumchota akili yule aliyewehuka upande wa pili. Baada ya maongezi aliyoyafanya katika simu hiyo iliyoingia punde, Alijinyanyua kitandani na kurudi maeneo ya kijitonyama sayansi nyuma ya kanisa. Eneo ambalo alikuwa akiishi mpenzi wake Bertha.
Baada ya kumaliza shughuli iliyompeleka. Saa saba ya usiku alirudi katika chumba chake, Keko magurumbasi. Alitumia taksi iliyompeleka. Ikamsubiri na kumrudisha mpaka Buguruni na yeye kuamua kuchukua taksi nyingine mpaka hapo. Sasa akawa anautafuta usingizi akiwa na bia nane kichwani. Bia alizozinywa katika ile klabu ya usiku maarufu kwa jina la kimboka by night. Hapo kulikuwako na madada poa waliouza miili yao kama ndafu ya shereheni.
Usingizi ukamkubali.
Licha ya usumbufu wa kunguni na mbu wa usiku alioupata, unadhani hata alijigusa? Lah! Aliyafurahia maficho yake. Japo usingizi ulimpaa jirani na alfajiri. Hali hiyo ilisababshwa na jinamizi la mawazo lililokuwa likimnyonga. Mwanga hafifu wa jua la alfajiri uliojipenyeza katika dirisha la chumba chake, ndio uliyomfanya aamke kivivu huku akitanguliza kitambi chake. Hatua zake zikiwa nzito kuubeba mwili mfupi kiasi uliobeba kifua kipana na kitambi cha bia na nyama choma; zote kwake zilikuwa kheri, mpaka alipokifikia kioo kilichopachikwa ukutani.
Akashituka.
Nadhani alianza hata kuisahau sura yake. Aliyasahau macho yaliyokosa nguvu ya kope za juu na kusababisha kuwa kama anayetaka kusinzia. Hata hivyo haikua sura ngeni aliyokuwa anatazamana nayo. Akakumbuka kuwa macho hayo yalikuwa ya kawaida. Macho yaliyomuwezesha kumpora Bertha kutoka kwa rafiki yake, Yesaya. Kidevu chake kikatawaliwa na msitu wa ndevu. Lakini hiyo haikuwa sababu ya kuisahau miaka ishirini na nne aliyoifukia kwa kula na kunywa kwa anasa. Aligeuza macho kukitazama kitanda alicholalia. Godoro jembamba kama ngozi ya tembo, likamdhihaki. Akajitusi mama yake mzazi kwa hasira. Kisha kicheko kisicho na ladha yoyote ya raha kikauharibu uso wake. Akili yake ikaanza kutafakari yaliyotokea asubuhi ya siku ya jana, iliyomfanya apahame Osterbye na kuja kujificha huku vichochoroni, Keko Magurumbasi. Ghafla ulimi wake ukapata nguvu ya kuinua matamshi kadhaa “Bertha” aliita jina la msichana aliyefanya urafiki wake na Yesaya kuangamia. Msichana waliyesoma wote chuo cha mlimani, kitivo cha sheria. Msichana aliyeiiba nafsi yake na kuiyumbisha yumbisha kama mawimbi ya bahari. Aliikumbuka siku ya kwanza Bertha alipowasili chuoni hapo akitokea Nyegezi Mwanza. “Anha! Kumbe na wewe ni msukuma? Mimi ni mwenzio bwana, naitwa Moses” akalikumbuka Tabasamu lililoacha uchi kinywa chake na kuonesha meno yaliyojipanga na kufanya mpangilio sahihi katika kinywa cha Bertha. Kwa mara ya kwanza Moses alikiri kuushika mkono wa malaika ‘laivu’ waliposalimiana kwa kushikana mikono. Ila Bertha sasa si Bertha tena. Ingefaa utangulize jina jipya, kabla hujaamua kumuita Bertha. Bertha kwa sasa aliitwa marehemu. Maiti yake yalifichwa na Moses ndani ya chumba chake mwenyewe Bertha. Chini ya kitanda na kuhifadhiwa kwa kuviringishwa ndani ya mkeka. Hakika aliuwawa kinyama. Moses alifanya unyama zaidi ya mnyama. Unyama aliomfanyia binadamu mwenzake. Shingo yake Bertha haikutenganishwa na kiwili wili wakati alipochinjwa kama kuku na kisu kilichopoteza makali kwa kukatiwa nyanya na vitunguu; mpaka Moses alipohakikisha kumlisha masoksi machafu mdomoni ili Bertha asitoe sauti. Japo si Bertha pekee aliyekuwa maiti ndani ya nyumba yake. Rafiki yake Pamela pia, alipoteza roho yake kwa kutaka kutoa ushahidi polisi. Yeye aliuwawa kikawaida kwa sumu aliyoinywa ndani ya maji ya baridi. Ilikuwa ni sumu kali sana. Nyongo ya mamba waliovuliwa kutoka katika ziwa Tanganyika. Ilisagwa na kuwa unga baada ya kukaushwa sana. Pamela aliipoteza roho yake kwa kiu ya maji ndani ya dakika kumi tu. Baada ya kufanya yote hayo, Moses alikumbuka kufanya jambo. Alikaa uelekeo ambao mwanga wa taa ulimpiga na kutumia kamera yake aina ya Kodak, kukipiga kivuli chake mwenyewe. Baada ya kuridhika na picha aliyoipata, akatumia mashine ndogo ya kusafishia picha hiyo, picha ikatoka vile alivyotaka. Akatabsamu kwa kebehi, kisha nyuma ya picha hiyo akaandika maandishi haya ‘KIVULI CHEUSI’ akaiweka picha hiyo pembeni ya kichwa cha Bertha, alichokiweka ndani ya friji.
****
“si kawaida ya Bertha kuchelewa kufungua mlango” alijinong’oneza, baada ya kusonya muda mfupi uliopita. Pamela aligonga mlango muda mrefu, bila dalili yoyote ya kuja kufunguliwa. Alijishauri aondoke, lakini alikumbuka kuwa Bertha alimtumia ujumbe kuwa, anamualika katika sherehe. Sherehe yake ya kuvalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Moses. Hivyo aliamua kujikaribisha, baada ya kuona kuwa; mlango ulikuwa wazi.
Mara tu alipoingia ndani, alipigwa na butwaa. Butwaa ya nini kimetokea kwa Bertha. Alilakiwa na damu nzito, iliyoanza kuganda pale sebuleni. Alihisi miguu ikikosa nguvu ya kukibeba kiwiliwili chake. Kizunguzungu kikampepesua, akastahimili kiukakamavu asidondoke. Mapaja yakalowana kwa mkojo uliomchuruzika kiuwoga. Hakika hali ya sebule ilitisha. Macho yakavutwa na matone ya damu, yaliyodondoka mpaka kwenye friji. Alijikokota taratibu kwa mwendo wa kuvizia, mpaka kwenye friji hilo. Alipolifungua friji, hakuamini alichokiona. Kilikuwa ni kichwa cha rafiki yake, Bertha. Mdomoni akiwa na matambara machafu. Wakati huo ndipo, kile kitu alichokuwa akikizuia kwa muda mrefu, kikampiga mtama. Alianguka bila kupenda, Pamela akazimia. Zilipita dakika nyingi, mpaka alipoanza kuhisi kichwa kikimuuma kupita kiasi. Hakujuwa amezimia kwa muda gani na pia alikwisha sahau, kilichomfanya ajikute kaibusu sakafu kama anayekisujudia kichwa cha rafiki yake mrembo, Bertha. Friji lilikuwa wazi hivyo kichwa cha Bertha kilikuwa juu kikionekana. Ulikuwa ni usiku mzito uliomuogopesha kuendelea kutazama hali ya nyumba ya rafiki yake. Alipiga simu katika kituo cha polisi kwa kutumia zile namba, zilizotolewa kwa ajili ya usalama wa raia. Kwa kuwa simu yake haikuwa na salio aliamua kutumia simu ya Bertha.
“habari yako?”
ilijibu sauti ya upande wa pili, baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Pamela aliongea kwa pupa, bila mpangilio wa mtu wa pili kumuelewa vizuri.
“anti embu tulia!”
ilikoroma sauti ile, Pamela akatii. kisha sauti ya upande wa pili ilivuta tafakuri na ilipopata uhai, ikasema “unasema mauaji?”
kabla sauti ile haijamaliza, Pamela alidakia tena “rafiki yangu Bertha, wamemuua kinyama. Kichwa chake” sauti ile, ambayo Pamela aliifahamu vizuri, ikapata tena uhai. Pamela hakuweza kuigundua, kutokana na papara zake na kuchanganyikiwa.
“unasema mauaji yametokea hapo nyumbani kwa rafiki yako?”
Pamela akajibu kiutulivu huku akiwa analia “ndiyo afande” Pamela alichukuwa jukumu la kumuelekeza mtu aliyekuwa akiongea naye, bila kuulizwa.
“sawa usimueleze mtu yeyote mpaka tutakapofika hapo”
Pamela alipoitikia, sauti ile ilitoa onyo la mwisho “kumbuka usimwambie mtu yeyote mpaka tutakapofika hapo. Hata wazazi wake wala mtu wake yeyote wa karibu usimwambie, hiyo ni kutokana na usalama wako. Pia usiende popote” kisha alikata simu.
Pamela aliendelea kusubiri kwa dakika arobaini na tano zaidi. Muda wote hakuwasha taa wala kujigusa. Alitetemeka kiasi cha kuhisi joto kali, licha ya kiyoyozi kilichokuwa kikibadilisha hali ya hewa kwa fujo, kikifanya kazi yake kiufasaha. Alikwisha jikojolea mara mbili kwenye kochi alilokalia akakauka. Choo kilikuwa ni cha ndani, vipi aingie akutane na muuaji kajibanza?
Alijiuliza.
Akiwa katika lindi la mawazo, ndipo aliposikia kitasa kikishikwa na mlango kufunguliwa. Kutokana na giza totoro, hakuweza kumuona aliyeingia. Mapigo ya moyo yalimuenda mbio sana, jasho likamtiririka kwa wingi. Kivuli kile cheusi, kilichojitoma ndani ya nyumba bila hodi, kikawasha taa. Macho ya Pamela yakamtoka pima baada ya kumuona aliyeingia.
Alikuwa ni Moses.
“shemeji” kilio kikaanza upya “wamemuua rafiki yangu, amewakosea nini jamani”
Moses alimkumbatia Pamela na kumliwaza kinafki. Walikaa kwenye kochi, huku Pamela akimuhadithia Moses yote tangu Bertha alipomtumia ujumbe uliomfanya yeye kuja hapo.
“aliniambia upo naye, leo ulikuwa ukimvisha pete ya chumba” Pamela alimshitua Moses. Moses akamtusi Bertha kimoyomoyo. Pamela akaendelea kumueleza mpaka alipopoteza fahamu baada ya kukiona kichwa cha Bertha ndani ya friji. Moses hakuoneshwa kushitushwa na hadithi hizo zote zilizosindikizwa na kilio. Alinyanyuka na kuelekea jikoni. Pamela alikuwa huru kwa kuwa aliaamini sasa ana mtu wa kumlinda. Lakini laiti angejua, asingethubutu kuiuza roho yake kwa mkopo. Alimwambia Moses
“nimewataarifu polisi, lakini naona wanachelewa”
sauti ilimfikia Moses jikoni, naye akajibu “umefanya vizuri”
Moses alikuja na bilauri ya maji ya baridi yaliyotoka kwenye friji ya jikoni. “ahsante shemeji umejuaje nilikuwa na kiu? Yaani sijatoka kwenda popote kwa uoga” aliyafakamia maji hayo, bila kujua hila za Moses. Moses alimtazama huku akimcheka kimoyo moyo. Alijiambia
“kufa Malaya wewe, kamsalimie mbwa mwenzio” dakika tano zilikuwa nyingi. Tumbo lilianza kumsokota Pamela. Pamela alilia kwa uchungu huku akimtazama Moses aliyekuwa akitabasamu. Pamela Akagundua kuwa maji aliyoyanywa yaliwekwa sumu. Alijuwa kuwa, Moses alipanga kummaliza ili ushahidi upotee. Akiwa katika kuugulia, alimwambia Moses
“kwa nini unatuua Moses? Kumbe ni wewe ndiye uliyepokea simu yangu? Kwanini Moses unafanya hivi? Tumekukosea nini?”
Moses alicheka kifedhuli, akamwambia neno moja ambalo liliisindikiza roho ya Pamela katika umauti “Pole Pamela, ni ujinga wako ndiyo umekuponza. haukuwa katika njama hizi, lakini ni upuuzi wako. Nililazimika kuidaiveti namba ya Bertha ila nikupate muda utakaokuja. Sikujuwa kama utaitumia simu yake kuwapigia polisi, ila nilifahamu utanipigia kuniuliza nilipo na kunipa taarifa ya msiba. Lakni harakati hizi haziishii hapa naapa kukiangamiza kizazi chake chote, na umsalimie kuzimu uendako” si maneno yote ambayo Pamela aliyasikia, kwa sababu tayari alikwisha funga macho na roho kuiacha mwili. Moses alicheka kwa kejeli baada ya kuzikusanya simu zote mbili, simu ya Pamela na Bertha kisha kutokomea nazo baada ya kuacha picha yenye ujumbe wa kivuli chusi nyuma ya picha aliyojipiga mwenyewe.
*****
TUMEANZIA HAPA………

TEMBELEA PAGE YA UWANJA WA SIMULIZI
0 comments: