Showing posts with label michezo ulaya. Show all posts

TAIFA STARS VS IVORY COAST: WACHEZAJI WA IVORY COAST WAPIGANA NA KUFUNGIWA

0 comments
Wachezaji wawili wa Ivory Coast wametimuliwa kwenye kikosi kinachojiandaa na mchezo kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Tanzania unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Taifa siku ya Jumapili.
Mchezaji wa zamani wa Monaco Jean-Jacques Gosso Gosso, 30, ambaye kwa sasa anakipiga kwenye ligi ya Uturuki akiichezea Mersin na kinda la miaka 20 Abdul Razack wa Manchester City, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Charlton Athletic, walipigana siku ya jumatano wakati timu yao ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuja Tanzania usiku wa leo.
FA ya Cote D’Ivoire imesema kwamba adhabu nyingine zinaweza kufuatiwa kutegemea na kamati ya nidhamu itakavyoamua.


Wakati huo huo timu hiyo ya Ivory Coast imeshafika nchini na wamefikia kwenye hoteli ya Bahari Beach.

Read More »

LIONEL MESSI NA BABA YAKE WATUHUMIWA KUKWEPA KULIPA KODI YA PAUNDI MILLIONI 3.4

0 comments
clip_image002Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi ametuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha  £3.4million.
Mashataka yamefunguliwa dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona na baba yake mwendesha mashtaka wa kaskazini mashariki mwa Catalunya, mahala ambapo Messi anaishi.
Wote wawili Messi na, Jorge Horacio, wanatuhumiwa kwa makosa matatu dhidi yao kwa kudanganya taarifa juu ya ulipaji kodi ambayo inafikia kiasi cha £3.4m cha kodi ya mapato katika miaka ya 2007, 2008 na 2009.
Jaji katika mahakama inabidi ayakubali mashtaka ya mwendesha mashtaka kabla ya kesi kufunguliwa rasmi.

Read More »

PSG SASA KUPAMBANA NA REAL MADRID KATIKA KUVUNJA REKODI YA DUNIA KUMSAJILI BALE..

0 comments

clip_image001Bale yupo mapumzikoni Amerika, lakini anatakiwa na PSG, pamoja na kocha wake, Villas-Boas
KLABU ya Paris Saint-Germain inajiandaa kuipiga bao Real Madrid kwa kumwaga Pauni Milioni 85 kumsaini Gareth Bale.
Mabingwa hao wa Ufaransa, wanamtaka kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas na wanatumai wakimnasa awe kocha wao mkuu, itasaidia pia kumkamata kwa urahisi Bale, kwani atashawishiwa na kocha wafuatane Paris.
Pamoja na hayo, hata kama kocha Villas-Boas ataamua kubaki London, hawataacha mkakati wao wa kumsaini Bale kwa kulipa ada kubwa ya uhamisho.
PSG imetumia zaidi ya Pauni Milioni 200 kwa ada za uhamisho wa wachezaji tangu mwaka 2011 ilipochukuliwa nma mabilionea wa Qatar Sport Investments, kampuni inayomilikiwa na familia ya kifalme Qatari, na tayari wanataka kuvunja rekodi ya dunia ya usajili kwa kumsajili Bale kutoka Tottenham.
Kwa sasa rekodi ya dunia ya ada ya uhamisho wa mchezaji ni Pauni Milioni 80, ambazo Real Madrid ilitoa kumnunua mchezaji wa Manchester United wakati huo, Cristiano Ronaldo.
Mkurugenzi wa Michezo wa Real, Zinedine Zidane alisema: "Ikiwa klabu yoyote itakwenda kutoa ofa Spurs, itagharimu fedha nyingi, labda hata kuvunja rekodi ya usajili. Kuna klabu nne au tano ambazo zina uwezo wa kifedha, lakini si uvunja rekodi ya usajili kiasi hicho,".
Hizo ni pamoja na PSG, ambayo rais wake Nasser Al-Khelaifi, mwenye umri wa miaka 39, anayeiwakilisha familia ya kifalme Qatari na mchezaji wa zamani wa kulipwa wa Tenisi, yuko tayari kupambana na ofa yoyote itakayotolewa na Real.
Bale amekuwa babu kubwa msimu huu, akifunga mabao 26, aking'ara kwa kasi yake kubwa uwanjani kiasi cha kuwa bidhaa adimu katika kipindi hiki cha usajili cha majira ya joto.
Bale mwenyewe yupo mapumzikoni Florida na inafahamika na anasikilizia mustakabali wake. Anaishi na mpenzi wake Emma Rhys Jones na mtoto wao wa kike wa miezi nane, Alba Violet na angefurahi kubaki London kama Tottenham itaendelea kuwa katika mwelekeo sahihi.
Tottenham Hotspur star Gareth BaleGareth Bale
Bale akionyesha uwezo wake Busch Gardens huko Florida, Marekani Gareth Bale came face to face today with Optimus Prime, leader of the Autobots, and BumblebeeThrills: Bale on Cheetah Hunt at Busch Gardens, TampaBale akiwa Cheetah Hunt, Busch Gardens, Tampa, Florida
Bale atasikilizia hatima yake kujua wapi atakwenda kati ya PSG, Real na Manchester United kutokana na Tottenham itakapoamua kumuuza.
Kocha Villas-Boas anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Mwenyekiti Daniel Levy na anaweza kuamua kubaki iwapo  atahakikishiwa bajeti nzuri ya usajili.
Mreno huyo amekuwa na wakati mzuri White Hart Lane, lakini inafahamika wanatakiwa kutumia fedha kwa kusajili wachezaji wazuri wenye uwezo wa kushindana katika Ligi ya Mabingwa na kushinda mataji.
Inafahamika, Villas-Boas anatazamia kuboresha kikosi cha Spurs, kwa kumsajili winga wa Barcelona, Ibrahim Affelay.
Big money move: Zidane has conceded PSG will have to shell out a record amount to land BaleZidane anataka kushindana na PSG kuwania saini ya BaleBig money move: Zidane has conceded PSG will have to shell out a record amount to land Bale
Wakati huo huo, Villas-Boas anataka kuwauza Jermain Defoe na Scott Parker. Spurs pia inataka kumuuza Emmanuel Adebayor anayelipwa Pauni 100,000 kwa wiki sambamba na Tom Huddlestone na Benoit Assou-Ekotto.All change: Parker, Adebayor and Assou-Ekotto could all be heading out of White Hart Lane Parker, Adebayor na Assou-Ekotto wote wataondoka White Hart LaneAll change: Parker, Adebayor and Assou-Ekotto could all be heading out of White Hart Lane All change: Parker, Adebayor and Assou-Ekotto could all be heading out of White Hart Lane

Read More »

BARCELONA YATAKA KUMSAJILI TORRES AWE SUPER SUB CAMP NOU

0 comments
clip_image001Soma yote juu ya hii: Gazeti la michezo la kila siku la Catalan,  Sport  limeandika kwamba Barcelona inataka kumnunua kwa Euro Milioni 20 Torres
HAWATOSHI Messi na Neymar peke yao kuongoza safu ya ushambuliaji, Barcelona imeripotiwa kutaka kumnunua mshambuliaji Fernando Torres.
Gazeti la kila siku la Catalan, Sport limeandika kwamba Barcelona inataka kutoa Pauni Milioni 17 (zaidi ya Euro Milioni 20) kumnunua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anayekipiga Chelsea.

REKODI YA MABAO YA TORRES

Msimu Mabao
2012-13 22
2011-12 11
2010-11 10
2009-10 22
2008-09 17
Pamoja na hayo, Torres hatakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza bali atakuwa anatokea benchi kama super-sub.
Matumani ni kwamba, Torres atatengeneza uzito sawa na aliokuwa nao Henrik Larsson, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki enzia zake Nou Camp kwa kufanya vitu adimu akitokea benchi hususan alipotoa pasi za mabao yote Barcelona ikishinda 2-1 dhidi ya Arsenal katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2006.
Lakini Sport limemsifia Torres ni mshambuliaji wa uhakika ambaye anaweza kufunga mabao kati ya 20 na 25 kwa mwaka.
Glory goal: Torres scored against Barcelona at the Nou Camp in the Champions League semi-finals last year

Read More »

BAADA YA KAZI YA KUJIUZA KWA DADA ZETU HIV NDIVYO WANAVYO LALA EBU ONA HAPA.

0 comments

Read More »

CHELSEA NDIO TIMU YA MWISHO KUIFUNGA BARCA MABAO 4 KWENYE CHAMPIONS LEAGUE: MESSI ANA NUKSI NA MULLER

0 comments
* Mara ya mwisho mshambuliaji Lionel Messi kuichezea timu iliyofungwa mabao 4-0 ilikuwa dhidi ya wajerumani. Argentina ilipofungwa kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010. Pia siku hiyo kama ilivyokuwa leo Thomas Mueller, alifunga mabao mawili tena. 

 * Barcelona wameruhusu wavu wao kuguswa mara nne katika mechi ya Champions League kwa mara ya kwanza tangu walipofungwa 4-2 na Chelsea katika hatua ya 16 bora March 2005.

* Timu ya kwanza kuifunga Barcelona 4-0 katika michuano ya ulaya ilikuwa ni Dynamo Kiev katika hatua ya makundi mnamo November 1997.

* Hakuna timu iliyofungwa kwenye raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Champions League/European Cup kwa mabao manne kwa bila au zaidi iliyoweza kufuzu kuendelea raundi ya pili. 

* Barcelona walipiga shuti moja tu liloenga goli la Bayern leo, idadi ndogo zaidi katika Champions League msimu huu. 

* Katika mashindano yote - Barcelona hawajafungwa 4-0 tangu walipoonyoshwa na Getafe katika kombe la mfalme May 2007. Miaka sita iliyopita.

Read More »

PICHA NA VIDEO ZIKIMWONYESHA SUAREZ ALIVYOMPIGA MENO IVANOVICH, HIZI HAPA

0 comments
Katika mechi ya Jana kati ya Liverpool na Chelesea, Mchezaji Luis Suarez amewashangaza tena wapenzi wa soka baada ya kitendo chake cha kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika pambano la ligi kuu ya England ambalo liliisha kwa suluhu ya goli 2-2.

Hatua hii ya Suarez inatarajiwa kutolewa maamuzi leo na Chama Cha Soka England kutokana na tukio lake la jana ambalo muamuzi wa mchezo hakuweza kulitolea maamuzi yoyote kutokana na kupitwa nalo licha ya Ivanovic kulalamika.

Hii ni mara ya pili kwa Suarez kufanya kitendo kama hiki ambapo rekodi zinaonyesha kuwa alikwishawahi kungata pia kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal.

Read More »

JOSE MOURINHO AMTIMIZIA NDOTO KIJANA MSAFISHA MITAA ALIYESAFIRI KUTOKA MAREKANI KWENDA SPAIN KUONA EL CLASSICO - NA KUMPA KAZI REAL MADRID

0 comments

Soka ina muda mchache kwa stori za kugusa moyo siku za hivi karibuni, lakini kama kuna mtu anaweza akatengeneza stori za kugusa mioyo ya watu basi ni Jose Mourinho Special One.

Katika stori ya kusisimua, Meneja wa Real Madrid ameweza kuyabadilisha maisha ya raia mmoja wa Mexico kutoka kuwa msafisha stesheni za treni mpaka kuwa mmoja ya watu muhimu ndani ya timu yake.

Abel Rodriguez, 41, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kusafisha stesheni za treni jijini Los Angeles, alitumia fedha zake chache anazopata kupitia kazi kusafiri mpaka ulaya na kujaribu kuangalia El Clasico dhidi Barcelona mapema mwezi wa pili mwaka huu.
Bila kuwa na tiketi, au hata sehemu ya kufikia jijini Madrid, kijana huyo wa kimexico alikuwa na tumaini kwamba angepata nafasi ya kuuona mchezo huo mkubwa duniani pamoja na kuweza kukutana na wachezaji. 

Kibahati bahati, Rodriguez alifanikiwa kufika kwenye uwanja wanaofanyia mazoezi Real -Valdebebas training complex mara baada ya kufika Spain, akiwa na mpango wa kuwaona mashujaa wake wakiwa kwenye maandalizi ya mechi.
 
Hakuwa na namna yoyote ya kuweza kuruhusiwa kuonana nao, ingawa miezi michache zilizopita alifanya ya bila malipo kama kijana muokota mipira (ball boy) wakati Real Madrid wakiwa kwenye pre-season huko California, lakini hilo halikuwafanya walinzi wamruhusu kuwasogolea wachezaji wa Madrid.

Akiwa hana shilingi, hana pa kwenda huku matumaini ya kuwaona mashujaa wake kwenye El Clasico,Rodriguez alikuwa amejikalia pembezoni mwa barabara kwa takribani masaa matano - then miujiza ikatokea.

Rodriguez aliyezunguzishiwa duara akiwa ndani ya Old Trafford na Cristiano Ronaldo

'Ilikuwa ni miujiza nilimuona yule kijana,' Mourinhoanakumbuka kwa kuwaelezea Sports Illustrated. 'Nilimuona Abel akiwa amekaa pembezoni mwa barababa nje ya uwanja wa mazoezi.
'Nilikuwa naondoka kwenye gari la msaidizi wangu Rui Faria, na kulikuwa na watu wengi nje, lakini nikwambia Rui asimamishe gari, "Simamisha gari - ni yule kijana wa Los Angeles".'
'Amigo! fanya nini hapa?? Mourinho alimuuliza Abel akiwa ndani ya gari.
'Nimekuja kuwatembelea nyie,' Abel Rodriguez alijibu. 'Ni mara yangu ya kwanza kujs ulaya, na ndoto yangu ilikuwa kuja kuona mechi zenu. Hasa El Clasico.'
'Lakini zimeshaisha zote,'  Mourinho alisema. 'Unaishi wapi sasa??'
'Sijafanya chochote kuhusu jambo hilo,' Mmexico akajibu. 'Kipaumbele changu kilikuwa ni kuwaona nyinyi halafu ningepanga mipango yangu. Kama nisingewaona - ningeenda uwanjani kujaribu kupata tiketi. Na kama hilo lisingefanikiwa basi ningerudi nyumbani.'
 
Then Mourinho akaamua kumpangia Rodriguez ambayo Real walikuwa wanakaa kujiandaa na mchezo dhidi ya Barcelona na akampa tiketi ya VIP.

Lakini Mourinho hakuishia hapo.
Duties: Rodriguez helped lay out the Real Madrid strip before their Champions League tie at Old Trafford
Rodriguez aliwasaidia Real Madrid kuvaa jezi hizi kwenye mechi ya mtoano ya Champions League pale Old Trafford

Wakati wa chakula cha usiku kuamkia siku ya Clasico, Mourinho akampa ofa rafiki yake mpya Rodriguez ya kuwa mmoja ya wafanyakazi wa Real - kama mtunza vifaa wa muda wa Los Blancos - wakati zikiwa zimebaki siku mbili kupambana na Manchester United.

Mourinho alisema: 'Nilimwambia hakuna namna angerudi nyumbani kwao, nikamwambia nitaenda nae jijini Manchester akafanye kazi kama mtunza vifaa vyetu. Nilimwambia atusadie kwa mechi hiyo na atapata nafasi ya kushuhudia mechi kubwa ya ligi ya mabingwa wa ulaya ndani ya Old Trafford.'
Rodriguez alirudi chumbani kwake na kuchukua passport yake ili maandalizi ya kazi yake mpya yaanze kufanyika. Kwa kufurahishwa na kilichotokea akaanza kulia katika meza ya chakula waliyokaa wachezaji wa Madrid.

Siku chache baadae, alikuwa ndani ya Old Trafford, akiwa amevaa sare rasmi ya Real na akiwapangia jezi wachezaji ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Celebration time: Rodriguez also saw his beloved Real Madrid beat Barcelona in the Clasico at the Bernabeu
 Rodriguez alipata nafasi ya kuiona timu yake ya Madrid ikishinda dhidi ya Barcelona kwenye el clasico ndani ya uwanja wa  Bernabeu

Baada ya ushindi uliozua utata ndani ya Old Trafford, Rodriguez akijikuta ndani ya chumba cha Manchester United akikusanya jezi za wachezaji wa United zilizosainiwa na wachezaji wenyewe na akafanya hivyo pia kwa upande wa wachezaji wa Madrid.
Pia aliagizwa na Sir Alex Ferguson akamwite Mourinho kwa ajili ya utamaduni wao wa kunywa mvinyo kila baada ya mchezo unaowakutanisha.

Rodriguez alirudi nyumbani kwao LA na jezi zilizovaliwa na wachezaji kama Javier Hernandez, Mesut Ozil, Kaka na Michael Essien, na mmoja wa mpira uliochezewa siku hiyo.
 
Akikumbuka wakati akimuaga mkewe aitwaye Olga na watoto wake watatu wa kike huko LA wakati akija ulaya kujaribu kuiona timu yake aipendayo, Rodriguez alisema: 'Nilikuwa na mashaka sana juu ya kwenda ulaya, lakini ushawishi mkubwa ulikuja kutoka kwa mke wangu, ambaye aliniambia, 'Inabidi uende. Imekuwa ndoto yako kwa muda mrefu.'

Read More »

HATIMAYE LIONEL MESSI ATUMA JEZI YAKE KWA PAPA FRANCIS - ANGALIA NAMNA ILIVYOPOKELEWA NA PAPA MWENYEWE

0 comments
Wote ni raia wa Argentina. Wote wanapenda mchezo mzuri. Na sasa wote wanamiliki jezi ya mchezaji bora wa dunia Lionel Messi.

Imerekodiwa video kwenye maeneo ya Vatican juzi Jumatano ikimuonyesha Padri wa Vatican akimkabidhi Papa mpya wa kanisa katoliki - Papa Francia jezi iliyosainiwa na Messi wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Papa huyo mpya na wana Vatican.

Baada ya kubusu mikono ya kiongozi wake, padri Miguel Delgado Galindo alimkabidhi Pope Francis jezi ya Messi ambayo ilionekana kumfarahisha sana kiongozi huyo mpya wa kanisa katoliki duniani. 

Hii ilikuwa jezi ya pili ya timu ya soka ambayo Papa aliipokea ndani ya wiki hii, baada ya waziri mkuu wa Spain Mariano Rajoy kumkabidhi Papa Francis jezi ya Hipania mapema wiki hii.

Read More »