BARCELONA YATAKA KUMSAJILI TORRES AWE SUPER SUB CAMP NOU
Gazeti la kila siku la Catalan, Sport limeandika kwamba Barcelona inataka kutoa Pauni Milioni 17 (zaidi ya Euro Milioni 20) kumnunua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anayekipiga Chelsea.
REKODI YA MABAO YA TORRES
Msimu | Mabao |
2012-13 | 22 |
2011-12 | 11 |
2010-11 | 10 |
2009-10 | 22 |
2008-09 | 17 |
Pamoja na hayo, Torres hatakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza bali atakuwa anatokea benchi kama super-sub.
Matumani ni kwamba, Torres atatengeneza uzito sawa na aliokuwa nao Henrik Larsson, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki enzia zake Nou Camp kwa kufanya vitu adimu akitokea benchi hususan alipotoa pasi za mabao yote Barcelona ikishinda 2-1 dhidi ya Arsenal katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2006.
Lakini Sport limemsifia Torres ni mshambuliaji wa uhakika ambaye anaweza kufunga mabao kati ya 20 na 25 kwa mwaka.
0 comments: