PICHA NA VIDEO ZIKIMWONYESHA SUAREZ ALIVYOMPIGA MENO IVANOVICH, HIZI HAPA
Katika mechi ya Jana kati ya Liverpool na Chelesea, Mchezaji Luis Suarez amewashangaza tena wapenzi wa soka baada ya kitendo chake cha kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika pambano la ligi kuu ya England ambalo liliisha kwa suluhu ya goli 2-2.
Hatua hii ya Suarez inatarajiwa kutolewa maamuzi leo na Chama Cha Soka England kutokana na tukio lake la jana ambalo muamuzi wa mchezo hakuweza kulitolea maamuzi yoyote kutokana na kupitwa nalo licha ya Ivanovic kulalamika.
Hii ni mara ya pili kwa Suarez kufanya kitendo kama hiki ambapo rekodi zinaonyesha kuwa alikwishawahi kungata pia kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal.

0 comments: