BAADA YA KUAMBIWA AMSHAURI MUME WAKE AACHANE NA SIASA.., HII NDYO KAULI ALIYOTOA JOICE KIRIA
 My Hubby Henry Kilewo.
 Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote.
 Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa (nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).
 Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"
Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu  fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake  aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli  HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi  yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa  ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.
 Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.
Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA  MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano  Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu  yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????
My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.
Fans Wangu wote naamini mtakuwa  mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu,  Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA  ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE.
 

0 comments: