CHEKI HII NDO GARI AMBAYO RIHANNA AMEMNUNULIA MPENZI WAKE CHRISS BROWN KAMA ZAWADI KATIKA BIRTHDAY YAKE.

Katika kuhakikisha kuwa Breezy anafurahia birthday yake ya kutimiza miaka 24 May 4 mwaka huu, Rihanna ametumia paundi 700,000 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 1.7 za Tanzania kumnunulia gari mpenzi wake huyo aina ya ’2009 Mercedes-Benz SLR Stirling Moss’, limited edition ambapo ni gari 75 zilitengenezwa.



Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun: “Chris yupo Las Vegas na washkaji zake hivyo atapewa zawadi zake za birthday akirudi LA wiki ijayo.



“Rihanna ametumia zaidi ya sola mioni moja kununua zawadi kuu – a custom-made car,” kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa siti za gari hiyo zimeandikwa majina ya Chris.

0 comments: