Niolewe na yupi kati ya nimpendae ama anipendae?



Hi all,

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza, nipo njia panda.

Iko hivi, nina wachumba wawili. Mr. X na Mr. Y. Nilifahamiana na Mr. Y miaka mitatu iliyopita, hatukuwa marafiki ila tulikuwa ni watu tunaofahamiana tu kwamba huyu ni Mr. Y anafanya kazi somewhere na huyu ni Nyakwaratony anafanya kazi.somewhere.

Siku moja Mr. Y akaniomba tukutane mahali fulani ana maongezi kidogo, bila hiyana nikaenda na kumsikiliza, akaniambia ananitaka uchumba, sikumkubalia moja kwa moja ila nilimwambia anipe muda. Kiukweli sikuwa namfeel hata kidogo na mpaka sasa simfeel.

Basi baada ya mwezi hivi nikampa jibu kuwa haitowezekana. Alikubali kwa shingo upande, kisha kila mtu akaanza na hamsini zake. Lakini hakusita kunijulia hali kila baada ya muda fulani.

Siku moja nikakutana na Mr. X, Yeye simfahamu sana ila nafahamiana na kaka yake kwa muda.mrefu na kaka yake ndiye aliyenitambulisha kwake. Wadau nampenda Mr. X kupita kiasi ingawa yeye anaishi mkoani.

Tukirudi kwa Mr. Y, siku moja nilikuwa nina shida ya kitu fulani na mtu pekee aliyekuwa na chance kubwa ya kunisaidia. Nilimpigia na akanisaidia mpaka nikapata nilichotaka. Sasa Mr. Y akatumia huo mwanya kutaka kukumbushia ombi lake, nikamwambia haiwezekani kwani yeye hajaokoka.

Alichonijibu nikajikuta nachoka mpaka maini, eti hakuna shida mimi nitaokoka tu kama hicho ndio kigezo cha mimi kukupata wewe. Na siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya ibada, akaniuliza nasali wapi, kesho yake akawahi hata kunishinda mimi. Nilidhani ni masihara, kumbe mwenzangu kadhamiria. Na hivi sasa anajiandaa kubatizwa ilhali mimi sina feeling naye. mimi mawazo, akili na moyo vipo kwa Mr. X

NOTE: Sijawahi toa papuchi kwa hao wote.

Nishaurini mwenzenu nifanyeje.

Samahani kwa habari ndefu.

Wasalaam

Nyakwaratony!

0 comments: