AIBU:MKE AFUNANIWA AKIJUIZA ATUPWA JELA MIEZI 6 MUMEWE ATOA MACHOZ HADHARANI.

MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.
Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa macho.

Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni MUME wa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.
0 comments: