PASIPO NA NIDHAMU SHULENI, MATOKEO YATAENDELEA KUFUTWA KILA MWAKA

Wanataaluma  wengi  wanapinga  uamuzi   wa  serikali  kuyafuta  matokeo  ya  kidato  cha nne  kwa  madai   kwamba  hilo  siyo  suluhisho  la  la  tatizo ......

Wasomi  hao  wanadai  kwamba  hiyo  ni   njia  ya  serikali  kujisafisha  kisiasa  na  kukwepa  kujiuzulu  kama   njia  mojawapo  ya  kuwajibika....
Wakitoa  maoni  kwa  nyakati  tofauti, wanataaluma  hao wanaamini  kuwa, upungufu  wa  walimu, mgogoro  ulipo  baina  ya  serikali  na   walimu,  nidhamu  mbovu  shuleni   ( baada  ya  serikali  kuzuia  matumizi  ya  viboko), ukosefu  wa vitabu  na  maktaba  ndo  vitu vya  msingi   ambavyo vimesababisha  ubovu  wa  matokeo......
Miongoni  mwa  wanataaluma  waliopaza  sauti  hadharani  ni  Makamu  mkuu  wa  chuo  cha  Saint Augostine, SAUT....
Akiongea  katika kipindi cha Tuongee asubuhi  leo, Makamu mkuu wa chuo cha SAUT Father  Charles Kitima amesikika  akilaani  kitendo  cha  serikali  kuyafuta  matokeo   ya  kidato  cha  nne...
Kitima   alisema wanaosema mitihani  isahihishwe upya hawana vision ya nchi hii kwani wako Bungeni kupiga  madawati na kufundisha watoto matusi na  kwamba  hawana weledi wa kuongoza  nchi hii.

0 comments: