AIBU:MHADHIRI WA CHUO KIKUU ADHALILISHWA NA KUTEMBEZWA UCHI KISA PENZI LA MWANAFUNZI
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Delta State huko nchini Nigeria alijikuta katika aibu kubwa baada ya kuvuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama baada ya mwanafunzi wa kike aliyekuwa akisumbuliwa na Mhadhiri huyo kuamua kumfanyia umafia kwa kumuwekea mtego.
Hatua ya kudharirishwa kwa Mhadhiri huyo ilikuja baada ya mwalimu huyo kumtishia Tega na kumwambia kuwa atamferisha kama hata kubali kufanyanae mapenzi.Kabla ya hapo Mhadhiri huyo aliwahi kumtongoza mwanafunzi huyo lakini mwanafunzi huyo alimkatalia kata kata, baada ya kuona hivyo Mhadhiri huyo aliamua kutumia wadhifa alionao kwa kumtishia kuwa kama hato kubali kulala nae basi atamfelisha mtihani.
Baada ya kuona hivyo Tega aliamua kumkubalia Mhadhiri huyo na kumshawishi badala kwenda kwenye hoteli kuchukua chumba ni bora waende nyumbani alikopanga mwanafunzi huyo ili wapunguze gharama,kuona hivyo Mhadhiri huyo alikubali haraka na kwenda nyumbani kwa Tega bila kujua kuwa kuna mtego amewekewa kumbe kabla ya hapo Tega alikuwa amesha waambia majirani zake na wanafunzi wenzake kuwa atahakikisha anamrubuni Mhadhiri huyo mpaka akubali kuvua nguo akisha kubali tu anamuaga kuwa anakwenda chooni kisha anawapigia simu waje kumuumbua Mhadhiri huyo kwani milango yote alikuwa ameirudishia tu na alikuwa ameshawaelekeza chumba ambacho atakuwepo Mhadhiri huyo.
Basi baada ya kuwapigia majirani na wanafunzi wenzake walifika eneo hilo la tukio na kufungua milango kimya kimya na kufanikiwa kuingia ndani mpaka chumba alipo Mhadhiri huyo ndipo walipo fanikiwa kumkuta Mhadhiri huyo akiwa uchi wa mnyama kitandani na kisha kumtoa nnje na kumtembeza uraiani ili watu wajionee wenyewe nini baadhi ya wahadhiri hufanya kwa wanafunzi wa kike.
0 comments: