"SITAKI KUOLEWA KWA SASA, BADO NIPO NIPO SANA".. SHAMSA WA BONGO MOVIE

BAADA ya hivi karibuni mchumba wake anayejulikana kwa jina la Dickson ‘Dick’ kuukacha uchumba, msanii wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kusema anaogopa sana ndoa.
Akistorisha na paparazi wetu, Shamsa alisema japokuwa mwanamke yeyote anahitaji kuolewa lakini yeye anaogopa kuingia kwenye ndoa kwani wanaume ni watu wa kubadilikabadilika kama kinyonga ambapo huwanyima uhuru wake zao kwa kuwawekea sheria kali.
“Naogopa ndoa mwenzenu, wanaume ni watu wa kubadilikabadilika. Nasubiri ahadi ya Mungu kama ni mapenzi yake nifunge ndoa na Dick basi itakuwa kama siyo siwezi kulazimisha kwani hapendi niigize kitu ambacho siwezi kukiacha,” alisema Shamsa.

0 comments: