MAITI YANYOFOLEWA PUA NA MDOMO KABLA LA KUZIKWA...!!
MAITI ya mtoto mdogo imenyofolewa viungo na watu wasiofahamika ikiwa imehifadhiwa ndani ya nyumba ikisubiri kuzikwa.
Tukio hilo lilitokea juzi katika Kitongoji cha Nyasura, Tarafa ya Serengeti, wilayani Bunda mkoani Mara.
Ofisa Tarafa ya Serengeti, Justine Rukaka, alisema kuwa mtoto huyo Emmanuel Paul aliyekuwa na miaka mitatu, alifariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa mshipa wa ngiri.
Alisema baada ya kufariki, mwili wake ulihifadhiwa ndani ya nyumba yao, lakini cha ajabu kesho yake wakati wakitaka kuuzika waligudua mdomo na pua vilikuwa vimenyofolewa na watu wasiofahamika.
Rukaka alisema kutokana na hali hiyo, waombolezaji walilihusisha tukio hilo na masuala ya ushirikina, hivyo kuhamasishana kuchanga fedha kwa ajili ya kumwita mganga wa kienyeji waweze kumbaini aliyetenda uhalifu huo.
Muda mfupi kabla ya kukamilika kwa kazi hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Ferdinand Mtui alifika kutuliza hali hiyo, na mwili wa mtoto huyo kuzikwa
0 comments: