MASIKINI DUDE:APATA PIGO JINGINE TENA:
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
ZIKIWA zimepita siku chache tangu msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ afiwe na mama yake mzazi, Mwadodo Ramadhan amepata pigo lingine baada ya kufiwa na mama yake mkubwa, Joha Ramadhan Mtongwa.Akizungumza na paparazi wetu, Dude alisema mama huyo alifariki dunia Jumatano wiki hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na presha ambayo ilisababisha mshipa wa damu kupasuka.
“Nimeumia sana kwani hata mwezi haujapita tangu nilipoondokewa na mama yangu mzazi, nilidhani mama mkubwa atakuwa faraja yangu lakini na yeye ameondoka,” alisema Dude kwa huzuni.
Mwili wa mama huyo ulisafirishwa Alhamisi iliyopita kwenda nyumbani kwao mkoani Tabora ulikozikwa.
0 comments: