Mpenzi wa Balotelli awa kivutio huko Brazil.
Mpenzi wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Italia Fanny Neguisha ameonekana kuwa moja ya vivutio kwenye michuano ya kombe la mabara inayoendelea huko nchini Brazil. Fanny amekuwa akihudhuria mechi zote za Italia na usikuwa kuamkia leo alikuwepo uwanjani wakati Italia inacheza na Japan huku akiwa amevalia jezi ya Italia.
Kwa wasiomfahamu wanaweza kudhania kuwa mwanamitindo huyo ni raia wa Italia kwa uzalendo aliouonyesha akiwa uwanjani lakini yeye ni raia wa Ubelgiji . Uwepo wa Fanny uwanjani unaonekana kumsaidia Super Mario ambaye alifunga moja ya mabao yaliyoisaidia Italia kushinda 4-3.
Hivi karibuni Mario alimvika mpenzi wake Fanny pete ya uchumba yenye thamani ya paundi laki moja baada ya tetesi kuwa zimesikika juu ya wawili hao kuachana kwenye mataa.
0 comments: