UNAMKUMBUKA SWEBE SANTANA WA KAOLE SANAA GROUP??? TAMBUA ANACHOKIFANYA SIKU IZI KUSUKUMA MAISHA
Anaitwa Adam jina lake halisi, lakini ukienda mitaa ya Magomeni ukamuulizia kama Swebe Santana basi itakuwa raisi kumpata zaidi ya kuuliza jina lake halisi. Mkali wa Kaole sanaa group Mzee wa mabreka Swebe alikuwa kimya na kupotea kabisa kwenye vyombo vya habari. Hii hapa ndiyo exclusive access unaipata kupitia mtandao namba moja wa bongomovie hapa bongo.
BONGOMOVIETZ: Ukimya wako wa muda mrefu unatokana na nini?
SWEBE: Mawazo yangu yananiambia filamu ni kitu kikubwa sana, sitaki nibabaishe niwaongopee watanzania. Sifanyi movie zangu mwenyewe kwasababu nadhani muda unafika wa Swebe kuja na movie yake ya ukweli na sio babaisha. Nahitaji kufanya movie yenye kiwango chake nikizingatia ishu nzima ya story,location na wahusika sahihi. Yote hayo yanahitaji bajeti ya uhakika, kwa ufupi ukimya wangu bado nilikuwa nafikiria na kupanga mipango ya kufanya kazi nzuri. Hivi karibuni nitafanya kitu kama mambo yataenda kama ninavyotarajia..
BONGOMOVIETZ: So, inamaanisha kwamba muda wote huo haujafanya kazi yoyote ya filamu?
SWEBE: Nimefanya movie chache na baadhi Za watu kwenye scene chache sana nikizingatia mpango wangu wakuja kufanya movie yangu mwenyewe as main character.Nimeshiriki movie kama za marehemu Kanumba na baadhi chache, kazi mpya niliyoshiriki kwa kuisimamia kabisa kama director na kuigiza ndani yake inaitwa Dangerous Deal.
BONGOMOVIETZ: Kama haufanyi kazi za sanaa kwa kiasi kikubwa kipato chako kinatokana na nini?
SWEBE: Nimeandika story kadhaa na zimetumika kutengeneza movie, so hiyo ni sehemu mojawapo ninayojipatia kipato. Lakini pia nafanya shughuli mbili tatu zinazoniingizia kipato kuendesha maisha yangu na familia yangu.
BONGOMOVIETZ: Niambie kuhusu familia yako?
SWEBE: Mimi sijaoa, lakini nina watoto wawili. Mkubwa anaitwa Rahimu anamiaka tisa yupo darasa la sita na mdogo wake anaitwa Rahma anamiaka 8.
BONGOMOVIETZ: Maisha yako binafsi nje ya sanaa, Swebe ni mtu wa aina gani na anafanya nini hasa?
SWEBE: Mimi ni mtu simple sana na mpenda mabadiliko, najihusisha na kazi za kijamii sana. Mfano hivi sasa mimi ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa, pia pamoja na watu kadhaa tumefungua NGO inaitwa “Jicho la Matumaini”. Tunajaribu kuwarudisha vijana wa kike na wakiume ambao wako nje ya mstari ambao jamii inategemea wanhegekuwa. Pia tunajari watoto ambao walipitia mazingira magumu na kuathirika labda kiafya ay hata kisaikolojia kwa kujaribu kuwaweka katika mstari mzuri zaidi ya pale walipo.
BONGOMOVIETZ: Hadi sasa mshapata mafanikio gani nah ii NGO yenu.
SWEBE: Tushafanya vitu ambavyo tunadhani ni vidogo, lakini kwasasa tukishirikiana na kituo kimoja kipo wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza kwenye kituo kinaitwa Mitundi. Plan nzima ni kwenda na watu maarufu kutumia siku mbili kukaa na hao watoto. Lengo la kukaa siku mbili ni kutokana na mfumo uliopo wa kuwapelekea watoto juisi za kemikali na biskuti na kuwaacha. Tunaamini upendo ni zaidi ya hizo biskuti wanzokula siku moja na kuisha, ila muda tutaowapa itakuwa kumbukumbu kubwa na kurudisha ndoto zao tena.
BONGOMOVIETZ: Unaonaje jinsi sanaa ya maigizo inavyoenda hivi sasa.
SWEBE: Tulipotoka ni mbali, lakini naamini kila mtu anajua kuna vitu vinatakiwa kurekebishwa. Kimoja ambacho naamini kipo ndani ya uwezo wetu ni ishu ya kuongopea kwenye covers za movie zetu. Utakuta cover zinakuwa fake sana, binti anaonekana mrembo sana na kependeza tofauti na character yake ya uhousegirl kwenye hiyo movie. Mawazo yangu cover za movie zilete uhalisia wa ndani. Tuuze kazi nzuri ya wasanii,production na story, na sio kuuza covers tu.
BONGOMOVIETZ: Msanii gabi unapenda kazi yake sana.
SWEBE: Napenda kazi za wasanii wengi na naamini wanajua kazi lakini wanajisahau tu kama wanaweza. Lakini kwa watu ambao naamini wanajua nini wanafanya na pia kazi zao zinavutia sana ni ROse Ndauka,Monalisa,JB na wengine
BONGOMOVIETZ: Unaliangalia vipi soko la filamu?
SWEBE: Bado kuna uongo mwingi sana, hatuna wasambazaji bali kuna wanunua haki. Uongo kwa maana ya kwamba siri wanaijua wao lakini kwa macho madogo tu unagundua uongo wao. Hauwezi kuambiwa movie yako nzuri imeuza copy 20,000 tu. Nenda mbagala ambapo kuna watu zaidi ya laki 6,haujarudi hapa Magomeni,Kinondoni,Sinza,Kariakoo,huko KImara na Mbezi. Sasa hii ni Dar tu, vipi Mwanza,Arusha na Morogoro. Soko hakuna kabisa, maana ya soko ni kwamba wadau wakuu wapate kile wanachostahili. So, kwasababu wasanii hawapati basi maana yake hakuna soko.
0 comments: