AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUBAKA MBAYA ZAIDI NDANI YA MSIKITI....!!

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemhukumu Ahamad Fadhil (63), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani ya Msikiti wa ni Mwembe Mmoja, mjini hapa.

Hukumu hiyo ilitolewa na jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Obadiah Bwegoge, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.

Hakimu Bwegoge alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.
 
Alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watano ambao bila kuacha shaka, walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Alisema shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji, alidai kuwa siku ya tukio, saa nane 8:00 mchana, alikwenda msikitini hapo kuomba msaada kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.
 
“Nilipofika nilikutana na huyo baba akaniambia ni kiongozi wa msikiti, hivyo nilisubiri akanichangishie fedha kwa waumini wake,” alidai.
 
“Ndipo mimi nikaingia ndani ya msikiti upande wa wanawake kuswali, baada ya kumaliza kuswali, mzee huyo aliniita na kuniingiza ndani ya eneo lingine nikafikiri nakwenda kuchukua mchango, kumbe nakwenda kubakwa,” alidai msichana huyo mahakamani.

 
Alidai kuwa mshtakiwa alimpapasa sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba alijitahidi kukataa lakini aliishiwa nguvu na ndipo mshtakiwa alipotumia fursa hiyo kumwangusha chini na kuanza kumbaka.
 
Kwa mujibu wa msichana huyo, wakati tukio hilo likiendelea, alitokea mzee mwingine na kuwatenganisha na mshtakiwa wakati akiendelea kumbaka.
 
“Alimtoa juu yangu na huyo baba ambaye ni mshtakiwa na kuanza kukimbia, ndipo waumini wa msikiti huo walipomkimbiza na kumkamata na kuanza kumpa kipigo,”alidai.
 
Alidai kwmaba wakati huo alikuwa amezimia na kwamba alipozinduka alijikuta akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa Maweni.
 
Mshtakiwa alipopewa fursa ya kujitetea, aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa madai kwamba  waumini wenzake wanamchukia ndiyo maana walinimpeleka mahakamani.

Kadhalika, alidaim kuwa sehemu zake za siri hazifanyi kazi kwa muda mrefu hivyo alisingiziwa.
 
Hakimu Bwegoge alitupilia mbali utetezi huo na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela.

Awali, ilidaiwa  na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Athumani Mshana, kuwa Febuari 19, mwaka huu, saa 8:00 mchana, eneo la Ujiji, Manispaa ya Kigoma/Ujiji, mshtakiwa alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani ya msikiti wa Mwembe Mmoja baada ya swala ya adhuhuri na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

0 comments: