Apoteza fahamu kwa siku 10 baada ya kupokea simu wakati anaichaji
Unaweza ukawa na deal nyingi sana kiasi cha kukufanya ushindwe kuzima simu yako ya gharama/ya kawaida, na inawezekana kabisa kuwa muda mwingine unaipokea wakati ikiwa kwenye chaji na unapiga story freeesh tu, ni vizuri ukashtuka mapema kabla hayajakukuta yaliyomkuta huyu..
Wu Jian Tong ambae ni raia wa China ameripotiwa kupoteza fahamu kwa muda wa siku kumi baada ya kupata mshtuko mkubwa alipokuwa akipokea simu yake aina ya iphone ilikuwa kwenye charge.
Taarifa zilizotelewa mjini Beijing na kutafsiriwa na ZDnet zimeonesha kuwa dada yake Wu Jian amesema alikuwepo wakati wa tukio hilo July 8 na alimsikia kaka yake akipiga kelele “I’m getting Shocked”.
Kwa upande wa muathirika mwenyewe Wu Jian alisimulia jinsi alivyojisikia wakati wa tukio hilo, “nilisikia maumivu ya kitu kama sindano kikipenya kwenye vidole vyangu, kisha nikasikia mkondo wa umeme ukipita haraka kidoleni kisha mkononi na kwenye mwili wangu.”
Ripoti zinasema Wu Jian alifikishwa hospitalini akiwa hajitambui na akitokwa na mapovu mdomoni, lakini alipata matibabu na kupata nafuu zaidi baada ya siku ya tatu.
Kwa mujibu wa daktari, hata baada ya siku hizo tatu alikuwa hajitambui (coma) na akawa na tatizo la upitishaji mzuri wa hewa.
Daktari alisema bila shaka hali hiyo ilitokana na shot ya umeme “It was no doubt an electric shock.”
Kwa upande mwingine kumetolewa taarifa juu ya chanzo cha kifo cha mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23 ‘Ma Ailun’ aliyepoteza maisha nchini China kwa mtindo huo huo (kupokea simu aina ya iphone wakati anaichaji).
Kwa mujibu wa mtaalamu wa maswala ya simu Xiang Ligang, aliyekuwa anahojiwa mapema wiki hii na CCTV, inawezekana kabisa kuwa marehemu alikuwa anatumia charger fake ama aliyoinunua kwa mtu tu, ama charger ambayo sio ya kwenye simu aina ya iphone.
Mtaalamu huyo amesema inawezekana kabisa kuwa charger hiyo haikuwa na vifaa vya kutosha vya kuzuia/kuchuja umeme unaoingia kwenye charger, ama kama ilikuwa navyo basi vilishindwa kufanya kazi.
Hata hivyo kampuni ya Apple ikishirikiana na uongozi wa nchini humo wanafanya uchunguzi kubaini chanzo hasa cha matukio hayo.
0 comments: