DRC: M23 wadai kumshika mateka mwanajeshi Mtanzania.
KUNDI la waasi la M23 nchini Drc limedai kumkamata mtu mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Christopher George Yohana katika hati yake ya kusafiria akipigana sambasamba na jeshi la serikali FARDC kupambana na kundi la M23 katika maeneo ya kibati nchini DRC.
Msemaji wa kundi la M23 Vernnei Kazarama ameiambia sauti ya amerika kwa njia ya simu kwamba kijana huyo anayesadikiwa kuandikishwa na serikali ya congo kama mwanajeshi wa Tanzania amejieleza na kukubali kwamba anatokeo nchi jirani ya Tanzania. (HM)
Mapigano yenye ghasia kubwa yalitawala Jumatatu ikiwa ni mwendelezo wa ghasia za mapigano mapya yaliyozuka julai 10 huko kivu kaskazini na kulazimisha maelfu ya watu kukosa makazi na kutorokea nchi jirani ya Uganda.
Kazarama amesema kama serikali ya Tanzania itaomba kuachiliwa mwanajeshi huyo kutoka tanzania kwa njia ya kipiplomasia au kupitia shirika la msaba mwekundi M23 iko radhi kumwachilia huyu mateka huyo.
Jumatatu kundi la M23 ilisambaza hati ya kusafiria yenye majina kamili na utaifa wa mateka huyo ikidai kwamba inataka kutuma ujumbe kwa dunia nzima kwamba Tanzania inaisadia Drc katika uvunjifu wa amani.
Sauti ya ameriba bado inaendelea kuitafuta serikali ya tanzania ili kutoa ufafanuzi zaidi juu ya maelezo yaliyotolewa na kundi la waasi la M23
0 comments: