MAJANGA...FEZA KESSY AGONGANISHA MABWANA NDANI YA JUMBA LA BBA, NI BAADA YA KUNASWA AKIOGA NA NJEMBA NYINGINE AKIWA UCHI...!!
Shemeji yetu Mbotswana, Oneal amechukizwa na kitendo cha Feza Kessy kwenda kuoga na mwanaume mwingine.
Jana jioni, Feza ilimlazimu amuombe msamaha mpenzi wake huyo aliyeoneshwa kuumizwa roho na kitendo hicho.
.
“Umefanya tena leo asubuhi. Umeniacha kitandani na kwenda kuoga na mwanaume aliye UCHI. I was so disappointed”, alisema Oneal ambaye hata hivyo hakumtaja mwanaume huyo.
“What was wrong with this particular shower”, aliuliza Feza ambaye alijibiwa na Oneal,”He was naked”.
Wasiwasi wa Oneal ni kama vyombo vya habari vya Tanzania vikipata picha hizo zinazomuonesha Feza akioga na mwanaume mwingine bafuni na kuzitumia, jambo ambalo linaweza kutia doa mapenzi yao.
Mrembo huyo wa Tanzania alimuomba msamaha mpenzi wake na kisha kumkumbatia na kumbusu huku wakijifunika shuka gubigubi, kitu kilichomaliza hasira za Mtswana huyo
0 comments: