AFANDE SELE NAE AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA OMMY DIMPOZ KUMTUKANA ALBERT MANGWAIR
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele' amuombea msamaha msanii wa muziki Omary Faraja 'Ommy Dimpozi' kutokana na kauli yake aliyeitoa inayodaiwa kumkashifu marehemu Alberty Mangwea 'Ngwair'.
Msamaha huo umetokana na kauli aliyeitoa msanii Ommy Dimpozi kudai kuwa hawezi kufa maskini kama msanii Ngwair.
Afande Sele alidai kuwa kauli hiyo haikuwa mbaya ingawa watanzania hawakuilewa hivyo Ommy ametereza ulimi na anapaswa kusamehewa kama binadamu anapokosea.
Alisema kauli yake ilikuwa inamaanisha wasanii wanatakiwa wapate haki za msingi na siyo kutumiwa huku wengine wakiendelea kunufaika na wao kudidimia na hali ngumu ya kimaisha.
"Hatuwezi kuendelea kufanya hivyo mimi namuombea msamaha kwa watanzania kauli yake ilikuwa na lengo zuri ila ameshindwa kuifikisha vyema hivyo ameteleza inabidi tumsamehe ili mambo mengine yaendele" alisema Sele.
Wakati huo huo bado ile kauli anayodaiwa kuitoa msanii huyo Ommy Dimpozi' inaendelea kumtesa na kusababisha kushindwa kuwapa burudani mashabiki zake.
Ommy Dimpozi alipata wakati mgumu baada ya kufanyiwa fujo na mashabiki alipokuwa akifanya shoo pamoja na wasanii wenzake walioshiriki katika Tuzo za Kilimanjaro mwaka huu wakiwa mjini Dodoma.
Msanii huyo anadaiwa kutoa kauli hiyo hivi karibuni ambapo alisema hataki kufa masikini kama ilivyokuwa kwa msanii wa Hip hop Albert Magwear.
Kauli hiyo iliwachukiza baadhi ya mashabiki wa muziki waishio mjini Dodoma ambapo msanii Magwear alisoma na kukulia katika mji huo.
Msanii huyo atazidi kuwa na wasiwasi kwa baadhi ya mikoa atakayozunguka kufanya shoo zake ikiwemo mkoa wa Morogoro ambapo ndio familia ya msanii huyo inapoishi.
Alipotafuta na mwandishi wa habari hili kuzungumzia ishu hiyo Dimpozi alisema hayuko tayari kusema chochote kinachohusiana na shoo yake ya Dodoma na hataki kumzungumzia Magwear.
0 comments: