"MWANAUME MWENYE FEDHA NYINGI SIMTAKI, NAMPENDA MWANAUME MWENYE MAPENZI YA DHATI"... JAQUELINE WOLPER

Jack Wolper  mwigizaji wa filamu swahiliwood. MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu, kwa hiyo kwa kuwa nao si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya dhati kwake kwani mapenzi yao ni chumbani tu, lakini hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.
.
Jack WolperWolper Gambe katika pozi.
Jack WolperWolper Gambe msanii wa kike wa filamu.
“Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake alafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi lakini ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyesha jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake”, “Wengi watu wenye pesa zao kuna wakati wananiona nina dharau lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke ya mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi sasa kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe. Aidha kuna watu ambao uwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine wao si malaika wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengetiboy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.

0 comments: