CHRISTIAN BELLA KIZUZINI LEO NA KUKAGULIWA KWA SHUTMA ZA MADAWA YA KULEVYA

KIMENUKA! Ile skendo ya mastaa kudaiwa kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ imechukua sura mpya baada mwanamuziki wa dansi, Christian Bella ‘kutaitiwa’ uwanja wa ndege kwa takribani saa 2, Ijumaa Wikienda lina mkoba kwapani.


Christian Bella akisalimiana na kaka yake, Nico Bella baada ya kusachiwa katika uwanja wa ndege.
Bella alikutwa na ‘sheshe’ hilo hivi karibuni alipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea Sweden.
Bella alitua na ndege ya Shirika Uturuki ‘Tukish Airways’ majira ya saa nane na dakika 8, usiku mnene akiwa na mafurushi kibao huku akionekana na kitambi kilichodaiwa kuwatia shaka wanausalama ambapo alikaguliwa na mizigo yake kwa mitambo maalum.
 Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alimshuhudia Bella akizunguka kwenye mitambo ya ukaguzi huku abiria wengine wakimpita na kuruhusiwa kuondoka.
Bella baada ya kusachiwa.
Huku familia yake ikipata hofu na kupigwa na baridi, ilipotimu mishale ya saa 10:00 alfajiri ndipo Bella alipomaliza kukaguliwa na kutoka kwenye mlango wa abiria wanaowasili kisha kupokelewa na Mkurugenzi wa Bendi ya Diamond Musica, Ally Ocs ‘Didik One’ ambaye amemsajili kwenye bendi yake.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa maofisa wa usalama uwanjani hapo alisema: “Siku hizi madawa ya kulevya yamekuwa yakipenyezwa sana kwenye viwanja vya ndege hivyo hakuna mtu yeyote anayeaminika.
“Watu wanatumia njia mbalimbali, wengine wanameza, wengine wanaweka kwenye mizigo ndiyo maana mitambo yetu ilikuwa ikimsachi vizuri kila mtu na hasa huyo Bella ambaye kwanza alionekana kuwa na mafurushi mengi ‘then’ ametunatuna tumboni lakini bahati nzuri alipita salama kwenye mitambo yetu.”
Christian Bella (kulia) akilakiwa na wenyeji wake.
Hata hivyo, jamaa huyo alitoa tahadhari kwa mastaa waosafirisafiri nje kuwa kama ishu hiyo wanaifanya waache kwa sababu wakikatiza eneo hilo lazima ‘kiwanukie’.
Baadhi ya mastaa wanaotajwa kupenda kusafiri nje ya nchi ni pamoja na Khadija Shaibu ‘Dida’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ali Kiba, Jacqueline Patrick na wengine kibao.
Kwa upande wake, mwanamuziki huyo alisema yeye anachojua viwanja vyote vya ndege kukaguliwa ni jambo la kawaida.

SOURCE: GPL

0 comments: