FULL STORY YA SKENDO YA NGONO KATIKA KANISA KATORIKI (ROMA)

LILE sakata la madai ya uzinzi kulitikisa Kanisa Katoliki nchini bado ni zito ndani ya Parokia ya Kristu Mfalme Tabata  Kigango cha Kimanga, jijini Dar es Salaam, Uwazi lina sehemu ya pili ya mkanda huo.


Polycarp Kardinali Pengo.
Uchunguzi wa pili wa Uwazi uliofanywa kwa wiki mbili umefanikiwa kulinasa jengo la ghorofa analodaiwa kulijenga mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya kanisa hilo, Faustin Mchanuzi kwa ajili ya kumhonga ‘nyumba ndogo’ yake, Dorosta Kengeli. Ghorofa hilo lipo Tabata- Kinyerezi, Dar.
Awali ilidaiwa kuwa, fedha za kujengea mjengo huo wa kifahari, mwenyekiti huyo alizichota kutoka kwenye vyanzo vya mapato vya kanisa hilo.
Timu ya Uwazi kwa kushirikiana na vyanzo vyake makini, mwishoni mwa wiki iliyopita ilitia timu nyumbani kwa mwanamke huyo anayedaiwa ni hawara wa mwenyekiti wa kanisa hilo na kufanikisha kupata picha ya mjengo huo unaodaiwa kugharimu mamilioni ya shilingi.
Mwanamke huyo alipobanwa na Uwazi kuhusu kujengewa ghorofa hilo, alisema nyumba hiyo ni yake na kwa sasa anamtambua Mchanuzi kama baba wa watoto wake na si vinginevyo.
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati wa mazungumzo hayo nje ya mjengo huo, mwanamke huyo  alikuja juu na kuwataka waandishi wetu wamsubiri aingie ndani na kurudi kutoa ufafanuzi zaidi lakini cha ajabu alipozama alijifungia moja kwa moja.
Jitihada za mapaparazi wetu kuonana naye tena ziligonga mwamba baada ya kumtuma mtoto wake wa kiume kutoa ujumbe kwa waandishi kuwa wanatakiwa kuondoka kwa vile mama huyo asingetoka tena.
Katika toleo la gazeti hili No. 792 la Mei 28 hadi  Juni 3, 2013 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa;
UZINZI WATIKISA KANISA KATOLIKI.
Katika habari hiyo, mwenyekiti huyo alidaiwa kumhonga nyumba ya ghorofa nyumba ndogo yake hiyo. Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alidai mwanamke huyo si hawara yake bali alikuwa mke wa pili wa ndoa ya mwaka 1993 lakini waliachana baada ya kujiunga na kanisa hilo lililomtaka amwache mke mmoja. Mke wa kwanza alimuoa 1970.
Alisema alimwongezea fedha za ujenzi wa ghorofa hilo kwa vile wakati wanatalikiana, mwanamke huyo alishamzalia watoto watatu.
Lakini habari mpya kutoka kwa waumini wa kanisa hilo walihoji kwamba ilikuwaje mwaka 1970 Mchanuzi alimuoa mkewe wa kwanza kwa ndoa ya kanisani halafu mwaka 1993 amuoe Dorosta tena kwa ndoa ya kanisani wakati yule wa kwanza bado yu hai? Hivyo, wanaamini mke wa pili ni nyumba ndogo yake.
Kikristo, mume au mke akishafunga ndoa hakuna talaka wala ndoa nyingine mpaka pale mwenza mmoja atakapoaga dunia.
Mei 20, mwaka huu, waumini wa kanisa hilo walimwandikia barua Polycarp Kardinali Pengo wakimtuhumu mwenyekiti huyo na paroko wake wakamtaka kuingilia kati sakata la kanisa hilo.

GPL

0 comments: