KAULI YA RONALDO KUHUSU TETESI ZA KURUDI MANCHESTER UNITED
Winga wa klabu ya Real Madrid Mreno Cristiano Ronaldo ameondoa utata unaozunguka mustakabali wake ndani ya Madrid baada ya kuhusishwa na tetesi za kurejea kwenye klabu ya Manchester United .
Amezungumza na waandishi wa habari huko Indonesia anakofanya ziara za mambo ya kijamii na kusema pamoja na kuweka wazi hisia zake kwa Manchester United maisha yake kwa sasa yako nchini Hispania ambako anachezea Real Madrid .
Amekuwa mgumu kuongeza mkataba wake na Real Madrid ndio maana akahusishwa na stori kwamba anarudi kwenye klabu yake ya zamani Manchester United.
Hivi karibuni Rias wa Real Madrid Florentino Perez alifichua taarifa kuwa Madrid imefikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na Ronaldo taarifa ambazo mchezaji huyo alizikanusha kutumia ukurasa wake wa Twitter.
Klabu kadhaa zikiwemo Paris St Germain, Monaco , Chelsea na Anzhi Makhachkhala zimekuwa zikifuatilia maendeleo ya mustakabali wa Ronaldo huku zikiwa tayari kumwaga fedha kumnunua staa huyu.
0 comments: