MUHIMU KWA WADADA AMBAO AWAJAOLEWA NA WANAPENDA MAISHA YA NDOA SOMA HAPA
Usiolewe sababu rafiki zako wote wameolewa. Usiolewe sababu class mates zako wote wameolewa na wanawatoto. Usiolewe sababu umemaliza chuo, unaishi mwenyewe na unakazi nzuri. Usiolewe sababu kila mtu kanisani anakuuliza pilau tutakula lini. Usiolewe sababu wazazi wanataka kumuona mkwe na wajukuu. Usiolewe sababu wazazi na wewe mmechoka kuchanga sasa mnataka kuchangiwa. Usiolewe ili uonekane umeolewa. Usiolewe kwa sababu umepata ujauzito. Usiolewe sababu unaogopa kuzeeka ukiwa mwenyewe. Usiolewe sababu unaona umri unakwenda.
Olewa kwa sababu ni wakati wa Mungu wewe kuolewa, umempata mtu sahihi mnayependana kwa dhati, umeridhia kutoka moyoni bila kuwa influenced na kitu chochote.
Ni bora uendelee kuishi mwenyewe kuliko kuingia kwenye ndoa ya majuto. Mngojee Bwana na hakika hatakuacha wala hajakusahau.
0 comments: