MWEZI WA RAMADHANI WAMFANYA WEMA ABADILIKE TENA


KUFUATIA Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au maarufu kama Madam amebadilika na kuondoa vitu vyote visivyo vya asili mwilini mwake.
 


Wema alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii akionekana amekata nywele zote huku akiwa ameondoa kope za bandia na kutoa kucha alizobandika kuashiria kuuheshimu mwezi huu huku akibaki na kila kitu cha asili  yake.
 


“Mwezi Mtukufu ni wa kuheshimiwa na kuweka kila kitu pembeni, nafurahi kuwa hivi kwa maana hata kama nikifunga swala zangu zitapokelewa vizuri,” alisema Wema.

0 comments: