NIMEPOTEZA SIMU INA PICHA ZANGU ZA NUSU UCHI, MTU AIKOTA NA KUANZA KUZIWEKA FACEBOOK-HELP

Ni rafiki yangu Wa kike na siku kadhaa zilizopita alipoteza simu yake ambayo ilikuwa Na picha alizojipiga akiwa half naked,Na nyingine ni Full naked.
Kuna mjanja kaiokota akatafuta jina lake akalipata,kaingia Facebook akafungua new account akaipa jina la Huyo binti.
Anachofanya now ana-upload picha moja baada ya nyingine kila siku na amempigia simu huyu binti anamwambia ampe laki 3 ili asitishe zoezi Na kufuta hiyo account..
Binti kachanganyikiwa now sababu hana hela Na nyumbani wakijua ni bonge LA msala na aibu coz mzee ni noma Na ni kiongozi wa dini ukizingatia na huu muda wa Ramadhani.
Nimejaribu kuchati jamaa kupitia account hiyo alipokuwa online asubuh amesema yuko serious Na sasa anaanza na video clip zilizomo!
Naombeni michango ya mawazo tumshauri nini cha kufanya kuhusu hili,Na je kuna uwezekano wa kufunga account au hiyo kwa njia tofauti au kama kuna sheria kumkamata na kumshtaki jamaa coz only kilichopo ni namba yake tu.

0 comments: