SIMULIZI YA KUSISIMUA: KIVULI CHEUSI,SEHEMU YA PILI
RIWAYA: KIVULI CHEUSI
MTUNZI: Stallone Joyfull
SIMU: 0654 846084
SEHEMU YA PILI
Moses alicheka kifedhuli, akamwambia neno moja ambalo liliisindikiza roho ya Pamela katika umauti “Pole Pamela, ni ujinga wako ndiyo umekuponza. haukuwa katika njama hizi, lakini ni upuuzi wako. Nililazimika kuidaiveti namba ya Bertha ila nikupate muda utakaokuja. Sikujuwa kama utaitumia simu yake kuwapigia polisi, ila nilifahamu utanipigia kuniuliza nilipo na kunipa taarifa ya msiba. Lakni harakati hizi haziishii hapa naapa kukiangamiza kizazi chake chote, na umsalimie kuzimu uendako” si maneno yote ambayo Pamela aliyasikia, kwa sababu tayari alikwisha funga macho na roho kuiacha mwili. Moses alicheka kwa kejeli baada ya kuzikusanya simu zote mbili, simu ya Pamela na Bertha kisha kutokomea nazo baada ya kuacha picha yenye ujumbe wa kivuli chusi nyuma ya picha aliyojipiga mwenyewe.
*****
Bertha alipendelea sana kunywa supu wakati ambao anaamka. Hakuna mtu ambaye, halifahamu hilo. Ndio maana aliweka oda ya kutengenezewa supu ya ulimi na chapati mbili, katika pub iliyo jirani na kwake. Hicho ndio kilikuwa kifungua kinywa chake kwa leo. Ilikuwa ni baada ya oda aliyoiacha jana alipoitembelea Pub hiyo, akiwa na Moses. Pub inayojulikana kama GQ. Wapishi na wahudumu wa pub hiyo, walikwishazoea kumpelekea mpaka nyumbani kwake. Walimthamini kutokana na kuwa mteja wao mkubwa na kumfanya wa muhimu kwao. Leo ikawa zamu ya Eva kupeleka supu. “mwambie atusamehe sana, tulikosa ndimu” mpishi mkuu wa jiko, alisikika kwa mbali. Eva alijibu huku akiendelea kutembea “huo ni uzembe jamani, kila inapofika zamu yangu hamkamilishi breakfast yake. Mimi namuogopa sana Bertha jamani” alizipita nyumba kama tatu, ndipo alipoifikia ya Bertha. Hakushangaa kukuta geti lipo wazi, lakini alistaajabu kukuta mlango ukimzomea na nzi wengi wakimlaki kwa shangwe. Alibisha hodi mara tatu kana kwamba aliukuta mlango ulikuwa umefungwa. Alijikaribisha ndani, akiwa ananyata, huku akiendelea kuita “Dada Bertha nimekuletea….” Mdomo wake ukakosa stamina na kuropoka neno “mamaaaaa!!!!!” baada ya kuangusha sahani iliyobeba bakuli la supu na chapati. Alikwisha jikwaa mara tatu na kupiga yowe. Alipokuwa akikimbilia getini, huku akitazama nyuma; GQ alipaona mbali. Hakika Eva alipendeza kuwa mwanariadha. Kisigino kilibaki sentimita chache, kigonge kisogo kwa kukimbia. Alienda mpaka kwa mpishi mkuu, bila kujali hasara aliyosababisha ya kulikwapua sinia lililojaa maini na chapati za mteja. “Mungu wangu…. Eva!!” muhudumu mwenzie alibwatuka, baada ya kushindwa kulizuia sinia lisianguke. Aliye angusha sinia, naye alimfuata Eva mpaka jikoni akipokimbilia. “Amekufa?” mzee huyo wa jikoni alibwatuka kwa butwaa. Hata Yule aliyekuwa akimjia kwa jazba naye aliuliza kwa kuhamanika “Bertha amekufa?” Eva alionekana kuchanganyikiwa kupitiliza “mimi jamani sifahamu ila nyumba yake haitamaniki, Kila sehemu damu; ila nilimuona amejilaza chini niliogopa kutazama kama ameshakufa au lah!” Eva hakujuwa kuwa Yule aliyemuona ndani ya nyumba ya Bertha, hakuwa Bertha bali ni Pamela. Mpishi mkuu wa jikoni alimuamuru Bosco, Yule mhudumu wa vinywaji; akaangalie nini kimemkuta Bertha. Kama kuna msaada wowote unahitajika, inabidi waitaharifu polisi. “sawa babu bonge” Bosco alijibu akitoka yeye na Eva mpaka nyumbani kwa Bertha. Bosco hakuamini alichokikuta ndani ya nyumba ya Bertha. Ilikuwa ni uvundo wa harufu ya damu iliyoanza kunuka. Aliziba pua yake na kuingia ndani. Alimuacha Eva nje, akitetemeka kwa uoga. Mwili wa Pamela uliojilaza sakafuni haukuwa na damu zaidi ya mapovu yaliyomtoka kutoka mdomoni. Bosco hakuitaji ushaidi wa daktari, kumuhakikishia kuwa aliugusa mwili tu, roho haikuwepo tena ndani yake “huyu siyo Bertha” Bosco akasema kwa nguvu. “sasa atakuwa nani bwana?” Eva alisema huku akichezesha chezesha miguu yake kwa uoga. “sijuhi ni nani? Na hizi damu ni za nani? Maana huu mwili hauna jeraha lolote” alisema Bosco. Jambo lililomvuta Eva kuingia ndani na kuangalia alichokuwa akikisema Bosco. Bosco yeye alikwisha ona damu zilizochuruzika mpaka kwenye friji, hivyo wakati Eva anaingia na yeye alikuwa amekwisha fungua mlango wa friji na kukiona kichwa cha Bertha, kilichong’ata matambara machafu. Miguu ikamkosea adabu, Bosco akadondoka kama mtoto aliyeanza kujifunza kutembea. Ilikuwa ni hali inayotisha. Eva alishitushwa na kuzimia huko kwa Bosco, akavutwa kukitazama kilichomfanya Bosco adondoke. Yeye alitapika , alitapika sana mpaka akaitapika nyongo. Mkojo ulimtoka na machozi kumchuruzika asijue ni hatua ipi ya kuichukuwa. “Berthaaa” alipiga mwereka alipotaka kukimbia, kumbe alimkanyaga Bosco aliyedondoka. Alijiinua na kukimbia hovyo kurudi GQ.
*****
Yeye Moses aliirudia taswira yake ile ile aliyokuja nayo jana. Kofia ya kizee vijana wakaiita pama, miwani mikubwa iliyobebwa na mashavu yake pamoja na jino moja la dhahabu. Taswira iliyomfanya aonekane mzee kwa kuvaa midabwada na mandevu ya bandia yaliyochafua kidevu chake. Alipanga hila za kutoka katika Guest hiyo ya vichochoroni, asigundulike na mtu wapi aelekeako. Ni Yule kijana mroho wa mapokezi ndiye aliufahamu ugeni wa Mzee huyo aliyejiandikisha katika kitabu cha wageni kwa jina la Mussoline. Mzee aliyenuka umasikini lakini mwenye pesa nyingi. Alijisemea hivyo Yule kijana. Moses alipopita pale mapokezi akiwa katika mwendo wake ule ule wa kuchechemea, Yule kijana alimsimamisha. “mzee umedondosha kitambulisho chako” Moses alikuwa ameshampita pale alipokuwa anafagia. Yule kijana alikuwa ameshakisoma kile kitambulisho na kuitazama picha ya muhusika. Hakuwa “mzee mussoline” alijisemea yeye. Moses alimshukuru na kumuondoa wasiwasi “nashukuru sana kijana wangu. Hiki ni kitambulisho muhimu sana” Moses hakujuwa Yule kijana alikwisha kisoma. Alimuuliza “sasa babu, huyo pichani ni nani?” Moses alishituka lakini hakumuonesha wasiwasi. Alimjibu kwa hekima, baada ya kikohozi kifupi kumpitia “mwanangu, mwanangu mpendwa na wa pekee Fredy. Amekufa katika kifo cha kusikitisha sana. Ndio maana nimekueleza ni kitambulisho cha muhimu kwa kuwa ni ukumbusho wa pekee unaonifanya nihisi ninaishi naye mpaka sasa” Moses aliongeza hila zake kwa kujifanya akivuta kamasi na kuyafuta machozi ya uongo na kweli kwa kitambaa. Alimuuliza “kijana, unaitwa nani tena?” yeye akajibu “pole sana mzee, mimi naitwa Omary au alimarufu kama Kibanga” Moses na Omary wakaagana kuwa wangeonana jioni wazungumze megi. Safari ya Moses ilikuwa ni kwenda katika ofisi za baba yake Bertha, akiwa katika Taswira ile ile. Kabla ya kwenda aliingia katika kibanda kimoja cha TTCL na kutumbukiza sarafu kadhaa na kuzungusha nambari za Mzee Raymond baba yake Bertha. Alizifahamu. “Raymond Chilambo nikusaidie nini?” sauti katika spika ilikoroma baada ya kuita kidogo tu. Moses alicheka kimoyo moyo baada ya kusikia sauti iliyopwaya kutoka upande wa Raymond. Yeye alijibu “hiki ni kivuli cheusi, ninakuja kuichukuwa roho yako” kisha alikata simu
*****
Bosco ndiye alipewa jukumu la kuitaarifu polisi. Alipiga simu ya mkuu wa kituo cha Osterbye, inspekta Nyaluto. “tupo njiani, ahsante kwa taarifa”
Nyaluto hakuwa mwenye maneno mengi. Aliikata simu baada ya kuelekezwa eneo lilipotokea mauaji hayo. Kifo cha Bertha kikawa gumzo katika maeneo yote ya Kijitonyama. Hata wasiomjua walipozisikia habari za kifo cha kinyama alichofanyiwa mrembo huyo, wakinamama kanga ziliwavuka kuelekea alipokuwa akiishi Bertha. Huyu akasikitika, Yule vinyweleo vikamsimama wengine walishika midomo yao. Kuna walioshindwa kuyazuia machozi yasiwaadhiri, kwa huruma waliyolaaniwa nayo wanawake, hata yakawadondoka. Ni nani ambaye asingeshituka kusikia “kichwa chake kimekutwa ndani ya friji, kikiwa kimetafuna soksi?” ilikuwa ni habari ya kusikitisha, iliyowavuta pia na waandishi wa habari. Waandishi wakataka kufahamu kuhusu maiti nyingine iliyopatikana ndani ya nyumba hiyo. Maiti iliyoonekana kuwa na kichwa chake, isiyo na jeraha lolote lililovuja damu. Kikawa kitendawili kwao Betha ni yupi na huyu ni nani? Hakuna ambaye aliifahamu familia ya Bertha, hivyo hakuna ambaye alitoa wazo la kumtaarifu ndugu au jamaa yeyote wa karibu na Bertha. Jeshi la polisi lilikuwa eneo la tukio, kupima hiki na kukiokota kile. Mwili wa Pamela uliwekwa ndani ya mfuko maalumu baada ya kupigwa picha kadhaa. Inspekta Nyaluto alikuwa karibu na Bosco kumuuliza ile na lile
“sasa huyu ndiye Bertha?”
Bosco akajibu “hapana, ila kichwa mlichokikuta kwenye friji ndiyo cha Bertha”
“kiwiliwili cha Bertha kiko wapi sasa?”
Ukimya wa Bosco ukamsuta Inspekta Nyaluto, akajuwa kuwa, Bosco hakuwa akijuwa lolote. Punde askari mmoja alisikia akipiga yowe kutokea katika chumba cha Bertha baada ya Harufu iliyomvuta kudadisi kulikuwa na nini dani ya mkeka uliofungwa kwa nyaya za umeme. Mkeka huo aliutoa kutoka chini ya uvungu. “kiwiliwili chake nimekitoa kutoka kutoka chini ya uvungu” alisikika akisema hivyo. Askari walifanya kazi hiyo pamoja na mpelelezi aliyeaminika sana katika kutatua matatizo mbalimbali yaliyowashinda makamanda hata wale wa jeshi. Yeye alijulikana kama Vanessa. Ni nani aliyesahau kuwa huyu ndiye mwanamke shujaa mwenye hekima, hata akakitoa kitanzi katika shingo ya Ramon? Ramon aliyezua gumzo katika jiji la Dar es salaam baada ya kuonekana kuwa amemuuwa mpenzi wake. Beatrice mtoto wa kigogo kutoka umoja wa mataifa, kama kesi hii ilivyo? Ditektivu Jafari Hiza alimnong’oneza Vanessa “hizi kesi za mpenzi kumuuwa mpenzi zinaelekea kukuandama sana Vanessa” kama kawaida yake, tabasamu likamponyoka. Muda mwingine unaweza usielewe alitabasamu nini. Lakini uzuri wa Vanessa ulimfanya aonekane anatabasamu hata kama hajatabasamu. Huyo ndiyo mwanamke aliyemfanya mwandishi aliyekunwa na njaa iliyomsumbua tumbo hata akadiriki kumfuatilia Vanessa kwa ukaribu na kuibuka na mkasa mzima ambao yeye mwandishi huyo, aliyejulikana kwa jina la Stallone Joyfully, aliamua auite NENDA NA MOYO WANGU. Vanessa alimtafuta mtu wa kwanza kugundua mauaji, ndani ya nyumba ya Bertha. Haikumchukua muda mrefu, kuletewa Eva aliyekuwa hajiwezi kwa kulia. Alimtazama kwa tuo kabla ya kumpatia leso ya kujifuta machozi.
“naitwa Vanessa” alijitambulisha
“naitwa Eva” kilio kikapamba moto
“naomba unyamaze nina maswali machache ninataa kukuuliza”
“lakini afande mimi sijaua” Maneno hayo ya kiudhaifu yakamponyoka Eva. Vanessa alicheka kwa huruma na kumwambia “usiogope, mimi sio afande ndio maana sijajitambulisha kama Afande Vanessa. Naomba uwe huru kuzungumza na mimi” alimpa moyo kisha aliendelea “naomba nifahamu wewe unamfahamu vipi Bertha”
jina lake alikwisha ambiwa na wakazi wawili, watatu wambea walioponyokwa na maneno wasiyoulizwa na mtu ambaye hawamfahamu. Ili mradi ilikuwa ni siku ya majonzi, kila mtu alizungumza lake analolijua kumuhusu Bertha. ‘alikuwa mpole, masikini dada wa watu’ alimsikia mmoja akisema . huyu naye “aliongea na kumchangamkia kila mtu” wa mwisho kabla hajamuita Eva ndiye akalitaja jina la Bertha “halafu Bertha ni mgeni, hapa hana hata wiki tatu. Yule jamaa yake aliyekuwa naye jana hapo GQ simuoni hapa? ina maana hana taarifa” pia habari hiyo ilimsukuma haswa afanye mahojiano na Eva.
*****
ITAENDELEA.....TOA MAONI YAKO!!!

TEMBELEA PAGE YA UWANJA WA SIMULIZI
0 comments: