JOKATE, MUSSA KIPANYA WAZUA JAMBO
MWANAMITINDO na mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mtangazaji Mussa wa runinga wamezua jambo kufuatia picha zinazodhihirisha urafiki wao uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi kunaswa.
Baadhi ya wadau walioziona kwa mara ya kwanza, waliibua minong’ono kuwa urafiki wao ni wa siku nyingi hivyo kuna uwezekano wakafikia hatua ya ndoa.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ katika pozi na Mtangazaji Mussa.
Awali paparazi wetu aliinasa picha ya wawili hao ambayo kwa mujibu wao, walipiga miaka kumi iliyopita na walipokutana tena mwaka huu wakapiga mpya.Baadhi ya wadau walioziona kwa mara ya kwanza, waliibua minong’ono kuwa urafiki wao ni wa siku nyingi hivyo kuna uwezekano wakafikia hatua ya ndoa.
Musa na Jokate katika picha ambayo inadaiwa kupigwa miaka kumi iliyopita.
“Urafiki wao ni wa kitambo, wanaweza kuja kuoana kabisa sababu aina ya maisha yao ni ya usiri sana,” alisema mdau mmoja ingawa wenyewe wamesema hawana cha kuzungumza juu ya hilo.
0 comments: