HUYU NDIYE MWANAUME PEKEE AMBAYE HAJAWAHI KUOGA WALA KUKATA NDEVU

Mr Singh na Mkewe
Hakika haya tunaweza kuyaita mafanikio ya ajabu kwa mzee huyu kutokana maamuzi yake.Labda tumite Mr Adui wa Maji ila jina lake kamili ni Mr Kailash Singh akiwa na ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu anayenuka zaidi kutokana na kutokuoga kwa zaidi ya miaka 37 sasa.

Mr Singh, 65, hajaoga na hata kukata nywele zake zenye urefu wa futi 6 toka mwaka 1974, mda mfupi mara baada ya kutoka kuoa.

Akielezea juu ya uamuzi wake wakushangaza, Mr Singh anasema mchungaji alimuahidi zawadi ya mtoto wa kiume kama atafata ushauri.

Licha ya majirani kuwa wanamtania na kumdhihaki jamaa huyo walishindwa kubadili maamuzi yake na namna ya kipekee alifanikiwa kumshawishi mke wake, ila cha ajabu zaidi ni pale ambapo imani yake imeonekana kumdanganya kwani ameishia kupata watoto saba ambao wote ni wa kike.

Source:Dan Chibo

0 comments: