Unyama: Binti aoza sehemu za siri amiminika usaha, baada ya kubakwa na kulatiwa
Mabinti wa kazi ni sehemu ya familia zetu kutokana na majukumu ya nyumbani tunayoawaachia ikiwemo mapishi,malezi ya watoto,uangalizi wa nyumba n.k. Tunaaswa kila mara kuishi nao vizuri maana nao ni binadamu na wanahitaji upendo. Si kila mtu analitambua hili,ukatili na unyama kwa mabinti hao umeendelea kushika kasi kila kukicha!
Binti mmoja (jina tunalo) kutoka Mtwara aliyeletwa Dar es salaam kuja kufanya kazi amejikuta kwenye mateso makali baada ya kutelekezwa bila nauli na kukutana na fataki aliomshawishi na kumuweka kinyumba na kusababisha majanga hayo yaliyofanya nimweke kwenye blog hii.
Akizungumza na Hatua Tatu ya Times fm Binti huyo amesema,Akiwa na umri wa miaka kumi na tano (15) tu, alitolewa kwao Mtwara na kuletwa hapa Dar na dada mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Sophia kwa ajili ya usaidizi wa kazi za ndani.Kwa maelezo yake ilitokea siku alimchapa mtoto wa bosi wake ndipo bosi alipokasirika na kufikia hatua ya kumtimua bila ya kumpa nauli ya kurudia kwao.
Alikutana na baba mwenye mke na watoto wa nne akamshawishi atampa maisha mazuri, akamweka kinyumba na kuanza kumtumia kimapenzi kinyume na maumbile. Kutokana na umri mdogo alionao,ilimsababishia kuharibika sehemu zake za siri na baba huyo na kumtelekeza baada ya kumtomlipia kodi sehemu aliyompangia chumba na majirani wa hapo ndio waliomsaidia.
Hivi sasa binti huyo ameoza sehemu zake za siri anamiminika usaha tu na amehifadhiwa hospitali ya Amana anakopatiwa matibabu na misaada midogo kama chakula.Cha kusikitisha zaidi baada ya kupimwa kakutwa na Ujauzito wa miezi mitatu na kapimwa virusi vya UKIMWI ambapo Vipimo vinatoka leo alhamisi kujua kama kaathirika au la.
Baada ya leo nitakupa jibu nini kimeendelea kuhusu vipimo na jinsi ya kumpa msaada binti huyu. Pia unaweza kumsikiliza leo Alhamisi na kesho kupitia Radio Times ndani ya kipindi cha Hatua Tatu.
Source: mamuafrica

0 comments: