PREZZO AKATAA KUMUOMBA MSAMAHA DIAMOND PLATNUMZ KUPITIA TWITTER.STORI NZIMA HII HAPA


Rapcellency, Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kwakuwa anaamini hakuna alichomkosea na ni jambo la kitoto.
Akiongea jana  mchana kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, kinachoendeshwa Mzazi Willy M. Tuva, Prezzo amesema Diamond ndiye aliyemchokoza baada ya wasanii hao kutumbuiza mwanzoni mwa mwezi huu kwenye tamasha la Matumaini.
 
 Prezzo anadai aligundua kuwa Diamond alimponda kwenye magazeti ya Tanzania kuwa hamwezi kwa lolote kwenye muziki.
 
“Mimi sipendi kuwa na adui kwa sababu muziki unafaa kuleta muungano, sa me nikashangaa mbona huyu brother ananiingilia na huku sikumbuki kumkosea wala hatujawai kukutana ana kwa ana,” alisema Prezzo.

“Mtu yeyote anamjua Prezzo ni kama rattle snake, ukimchokoza you have to get prepared to be bitten.”
Rapper huyo aliendelea kudai kuwa alimpigia simu Diamond lakini hakupokea na ndio maana aliamua kumdiss kwenye Twitter.
  “Jamaa hakupokea simu nikaona ah! Basi liwalo na liwe, nikadecide ku-air my views.”
Hata hivyo Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kama anavyomtaka afanye.
 
“Unaona kwa saa hizi akianza kusema aende kwa Twitter aniombe msamaha, maisha huwa hayaendi hivo…kwa hivyo vitu vingine naona ni kama ni utoto unaingilia kati, kwani yeye kusema niombe msamaha kwa Twitter….niombe msamaha kwa kosa gani? Kusema ukweli,unajua mimini msema ukweli, mimi kuomba msamaha kwa Twitter naona kidogo ni utoto.”
Hata hivyo Prezzo amesema hataki beef na Diamond kwasababu anamheshimu na amemshukuru Willy Tuva kwa kujaribu kuwasuluhisha.

0 comments: