TID AFUNGUKA BAADA YA KUSIKIAKWAMBA Ali Kiba anasikilzwa zaidi Muscat, asema ni muda wake “It’s too late for this reminder it’s my time”

 Khalid Mohamed, Top In Dar (T.I.D) ambae pia ni mmiliki wa Top Band amepinga vikali taarifa zinazoonesha kuwa Nyimbo za msanii mwenzake Ali Kiba zinasikilizwa zaidi Muscat huenda kuliko msanii mwingine wa Bongo Fleva.

Taarifa hizi zilizotolewa na mtandao wa
Bongo5 ambao ulipata maelezo ya kina baada ya kuchat na mtanzania aishie nchini Muscat aliyetambulika kwa
jina la Rayya Al Habsi aliyewapa tathmini kuhusu nyimbo za kibongo zinazosikilizwa zaidi huko mjini Muscat,Oman.

Rayya alisema nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa sana lakini pia wasanii wengine wanaopendwa ni Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na Dully Sykes.

Rayya aitaja pia upande wa mduara kuwa ni AT, Off side Trick na Kilimanjaro Band, na kwamba band inayofunika zaidi ni Twanga Pepeta.

Taarifa hizi zinakuja wakati ambapo T.I.D amepata deal la kwenda mjini Muscat kupiga show akiwa na band yake ‘Top Band’, na hivyo ameona kama taarifa hizi zimepotoshwa na yeye ndiye alistahili kutajwa katika nafasi aliyopewa ‘Ali Kiba.’ Na kwamba yeye ameshapiga show mara mbili na anaenda kwa mara ya tatu akiwa na band yake.

Kupitia ukurasa wake wa facebook T.I.D a.k.a Mnyama amedondosha  maelezo confidently.

“This came after I have been mentioned perfoming well its too late for this reminder its my time,and they listen to me alot its my third time perfomin there and this time with my band.”

Kisha akaambatanisha na kichwa cha habari chenye picha ya Ali Kiba kama kilivyoandikwa na Bongo5, yenye kichwa cha habari “Nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa zaidi Muscat ‘huenda’ kuliko msanii mwingine wa Bongo Flava.”

Well, yale yanaweza kuwa ni maoni ya Rayya, maoni sio utafiti rasmi japo unatoa picha ya jumla. Lakini inaonekana kama Top In Dar hataki kuwa Down any where hivi hivi.

0 comments: