YUSUF MLELA AFUNGUKA KUMRITHI SAJUKI KWA WASTARA

BAADA ya wiki iliyopita kumleta kwenu staa wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela ili mumuulize maswali, leo tunawaletea majibu na ufafanuzi wa maswali mliyomuuliza. SHUKA NAYO…
HUYU ANAMKUBALI
Mimi ninakukubali kinoma kwa sababu huna majivuno wala skendo kwa hiyo kaka endelea hivyohivyo. Calvin Mabula, 0719371176


MLELA: Asante.

ONGEZA UBUNIFU


Nakupa hongera kwa uigizaji wako lakini pia ongeza ubunifu, skendo usizipe nafasi hazitakujenga bali zitakubomoa. Kelvin Mwaibula, 0713644447

MLELA: Asante kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.


YEYE NA WASTARA


Mlela umeanzia mbali enzi zile ukiwa bado chalii, nakuombea heri uendelee kuwa nyota, fafanua kuhusu uhusiano wako na Wastara (Juma) maana tayari watu wanasema unataka kumrithi (Juma Kilowoko (Sajuki). Rocky, Moshi, 0715289337

MLELA: Wastara ni mtu wangu wa karibu sana tangu Sajuki akiwepo, tunafanya kazi pamoja ninampa sapoti kwani hana mtu wa kumsaidia kwa hiyo ni kazi tu hakuna mapenzi.


VIPI KUHUSU CHIPUKIZI?


Hongera sana kaka kwa kazi zako nzuri, ni kwa nini katika filamu zenu hamuwashirikishi wasanii chipukizi wanaosota ili kupata nafasi ya uigizaji wa filamu au filamu zenu zinakosa soko? Cecy Jose, Dar, 0752597199

MLELA: Filamu zangu nyingi nimewashirikisha chipukizi isipokuwa huwezi kuwapa majukumu makubwa kwa sababu bado wanajifunza.


JE, UMEOA?


Mlela kiukweli wewe ni msanii wa kitambo kunako gemu la filamu za Kibongo, je, vipi kuhusu kuoa au una mpenzi wa kujiliwaza tu? Salim Liundi, Dar, 0658110395

MLELA: Nina mchumba na masuala ya kuoa yapo njiani yanakuja.


ETI NI FREEMASON?


Mlela kuna tetesi kuwa wewe ni Freemason na uliambiwa masharti yake usiwe na skendo, vipi kuna ukweli gani ndani yake? Issa Chongono, Tanga, 0714455748

MLELA: Siyo kweli, hayo mambo siyafahamu kabisa.

HUYU ANAMHOJI?
Watazamaji wa filamu kwa sasa wanafahamu filamu mbovu na nzuri, unafikiri nini kifanyike kuboresha kazi zenu? Elia, Iringa, 0718085308
MLELA: Kikubwa ni kuwa makini, kujitambua, kuongeza umakini katika kazi na kutengeneza filamu bora zaidi ya hizi tulizonazo sasa. 
ANA UNDUGU NA HEMEDY?
Mlela ninakukubali sana katika kazi zako, ninachotaka kukuuliza ni hivi, wewe na Hemedy (Suleiman) ni ndugu? Cambiaso, 0714825056
MLELA: Hapana.
ANAWAEPUKAJE WANAWAKE?
Mimi ninakupenda kaka Mlela, kwanza una sauti nzuri sana, unajiheshimu, huna skendo kabisa za mademu na wewe ni kijana mzuri sana unayevutia, hivi unawaepukaje wanawake? Big up. Mukar Liber, Dar, 0652877883
MLELA: Asante, mimi ninajitambua kwani siendekezi wanawake, wakija kwangu huwa ninawaambia niko kikazi zaidi.
HUYU ANATAKA KUMFAHAMU
Kaka Mlela vipi wewe ni kabila gani, una miaka mingapi na una elimu gani, unajisikiaje unapoigiza na Hemedy? Msomaji, 0654941334
MLELA: Mimi ni Mnyamwezi, nina miaka 27, elimu yangu ni kidato cha nne, kuhusu Hemedy huwa najisikia kawaida tu kama ninavyoigiza na wasanii wengine.
HUYU ANAMSIFIA
Tunapozungumzia Bongo Movies basi wewe ni mfano bora kaka, kaza buti uzibe pengo la (marehemu Steven) Kanumba, nakukubali sana. Cindy, Dar, 0713663787
MLELA: Asante, ninashukuru.
ALIWAHI KUTOKA NA CLARA?
Mlela nakukubali sana, ulishawahi kutoka kimapenzi na msichana mmoja anaitwa Clara. Msomaji, 0716667231
MLELA: Simfahamu.
NJE YA FANI ANAFANYA NINI?
Mlela wewe ni msanii usiyekuwa na skendo na unafanya vizuri kwenye sanaa, je, mbali na sanaa unajishughulisha na nini? Msomaji, 0682683474
MLELA: Ninafanya biashara zangu ndogondogo.
ANATOKA NA ODAMA?
Napenda unavyoigiza, je, ni kweli unatoka na Jennifer Kyaka ‘Odama’? Msomaji, 0656673871
MLELA: Asante, Odama sitoki naye kimapenzi.
AMEANZA MAPENZI LINI?
Kaka umeanza mademu wakati gani na mwanamke gani wa Kibongo unamwelewa kuliko wote? KBZO, Mbeya, 0759887112
MLELA: Nilianza mwaka 2004, mwanamke ambaye ninamwelewa sana ni Zena kwani anajiheshimu na anajua nini thamani ya mwanaume.

0 comments: